NISHATI JADIDIFU KUPUNGUZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA:


 Na Doreen Aloyce, Dodoma


Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amesema Serikali itahakikisha kuwa Nishati Jadidifu itakuwa moja ya chanzo kikubwa cha kuzalisha nishati nchini ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira nchini.


Byabato ameyasema hayo, leo wakati wa Mkutano wa wadau wa Nishati jadidifu na uzinduzi wa miradi ya Nishati jadidifu,uliofanyika jijini Dodoma.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua miradi hiyo ya nishati jadidifu, alisema kuwa nishati mbadala ni nishati ambayo inafaida kubwa  ya kutochafua mazingira kwa upana wake na ina faida ya kutumika kidogo  na kufanya kazi kubwa.


“ tumezindua miradi miwili, mradi wa kwanza unaofadhiliwa Umoja wa Ulaya  lakini unapewa fedha na UN unalenga kuhakikisha kunakuwa na matumizi machache ya kuni na mkaa katika maeneo yetu, na mradi wa pili tuliozindua ni mradi unaolenga Zaidi kwenye kilimo lakini kwa kutumia umeme jua miradi yote hii imelenga katika matumizi sahihi ya nishati jadidifu”, alisema.


Alifafanua kuwa, mradi huo uliojikita kwenye matumizi ya  Nishati safi ya kupikia, utaanza kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na Mwanza ambapo imeelezwa kuwa katika  majiji hayo mkaa unatumika kwa kiwango cha juu kulinganisha na mikoa mengine,  ambapo  mkoa wa dar es salaam unaongoza kwa matumizi ya mkaa kwa  asilimia 50 ya mkaa wote unaotumika nchini.


Sambamba na hilo, alisema Wizara imejipanga kuhakikisha kuwa  mwaka huu inazalisha megawati 150 kutoka kwenye vyanzo  vya nishati jadidifu kwa maana ya jua na upepo na tayari Serikali imeanza kusaini mikataba na wawekezaji mbalimbali ili kuanza kutekeleza miradi hiyo.


Pia, Serikali imejipanga ifikapo mwaka 2025 kwa kutumia vyanzo mbalimbali ambavyo vipo nchini kuzalisha megawati 1100 zitokanazo na nishati jadidifu jambo ambalo litawezekana  kwasababu kunampiango  mizuri iliyopo na utekelezaji wake unaonekana.


Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Manfredo Fanti, alisema kuwa Mradi ambao umezinduliwa ni sehemu ya mashirikiano baina ya Umoja wa Ulaya na Tanzania kwa upande wa sekta ya nishati.

Aidha, alisema mradi huo ni muhimu kwasababu  utatoa mchango mkubwa katika kupunguza matumizi ya mkaa hasa katika maeneo ya mjini na vijijini.


Vilevile, amefafanua kwamba mradi huo hautasaidia  kupunguza uharibifu wa mazingira tu lakini pia utasaidia kuimarisha afya za watu kwakuwa hewa itokanayo na moshi wa matumizi ya  mkaa na kuni una madhara kwa afya ya mtumiaji.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post