Mgaya afungwa miaka30 kwa kumbaka Bibi kizee wa miaka70

 Na Mwandishi Wetu, Ludewa


Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elias Mgaya (20) mkazi wa kijiji cha Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kosa la kumbaka bibi kizee wa miaka 70.

Akisomewa hukumu hiyo jana na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 32 la mwaka 2021 Elias Mgaya ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 (1) (2)(c)na 131(1) Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

Awali akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asigile imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo machi 29 mwaka huu ambapo alimvamia bibi huyo(jina lake limehifadhiwa) nyakati za usiku akiwa amelala na kisha kutenda kosa hilo.

Katika hukumu nyingine Mahakama hiyo pia imemhukumu kifungo cha maisha jela George Lupindu(19) mkazi wa kijiji cha Ngalawale kwa kosa la kumbaka mtoto wakike mwenye umri wa miaka 9.

Akisomewa hukumu hiyo  na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 37/2021 Geaorge Lupindu ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura namba 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa Mapitio  mwaka 2019.

Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka Asifiwe Asigile kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai 7 mwaka huu ambapo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wakati akitokea shuleni kwa kumdanganya kuwa anampeleka nyumbani kwao na kisha kumkamata kwa nguvu na kutenda kosa hilo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post