Serikali yapiga marufuku uuzwaji wa malighafi ya shaba nje ya nchi


Na Doreen Aloyce, Dodoma 


SERIKALI imepiga marufuku uuzwaji wa  Shaba Chakavu (copper Scraps) nje ya nchi, na kuwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara hizo kufanya biashara hiyo nchiilni pekee.


Shaba ni miongoni mwa bidhaa ambayo hutumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za vyuma  hapa nchini ambapo katika siku za hivi karibuni imekuwa adimu jambo ambo limekuwa likisababisha kupanda kwa bei ya chuma sokoni.


Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila  Mkumbo ametoa agizo hilo jana, Jijini Dodoma  alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake akielezea tathimini ya mwenendo wa uzalishaji , usambazaji,na bei za vifaa vya ujenzi nchini kwa kipindi cha mwezi September mpaka Novemba mwaka huu.


Amesema kutokana na Nchi ya Tanzania kuwa na bidhaa zinazotokana na Shaba hasa mabati ambapo kwa hapa nchini Kuna viwanda viwili bidhaa hizo zimeonyesha kupanda Bei kutokana na kwamba wazalishaji wanategemea Nchi ya china kutafuta malighafi za kutengenezea bidhaa hizo ambazo zimekuwa adimu nchini China.


"Viwanda viwili vya kuzalisha mabati vina uwezo wa kuzalisha kwa mwaka mabati 14,949,703 sawa na Tani 200,000) kwa mabati ya geji 28 ambayo utumika zaidi hivyo kwa Mkoa wa Mwanza imepanda kutoka shilingi 31,700 kwa mwezi Septemba mwaka huu Hadi shilingi 33,400 mwezi novemba mwaka huu " amesema 


Kuwa upande wa Saruji  hapa nchini Kuna viwanda Tisa vyenye uwezo wa kuzalisha Tani 9,080,000 kwa mwaka na kwamba Bei za Saruji zimepanda kwa wastani wa shilingi 1,000 kwenye Mikoa ya mwanza ,Dar es salaam,huku Mkoa wa Ruvuma Bei ikishuka kwa asilimia  15 kutokana na kuwa karibu na kiwanda Cha Dang'ote .


"Pia tuna viwanda 16 vya nondo vyenye uwezo wa kuzalisha Tani 1,082,788 za ukubwa mbalimbali na kwa mwaka vinaweza kuzalisha wastani wa Tani 750,000 za nondo hivyo kama Serikali hatuna budi Kuzuia bidhaa ambazo zinatokana na haya malighafi kutokwenda nje ya nchi kwani hazitoshelezi "ameongeza.


Kuwa kutokana na hali hiyo Serikali inachukua hatua kudhibiti ongezeko lisilohalali la Bei za bidhaa muhimu nchini ikiwa kuhakikisha Wizara husika Kutoa taarifa ya mwenendo wa wastani wa Bei za bidhaa muhimu kila mwezi kwa Mikoa yote ambapo itawapa wahusika uelewa wa kutosha Kuhusu uhalisia wa Bei za bidhaa.


"Nawahimiza Tume ya ushindani kuendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa upangaji wa Bei nchini na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria wafanyabiashara ambao wanakiuka sheria ya ushindani nchini "


"Jambo lingine Serikali Katika mpango wa muda mrefu itatekeleza miradi kielelezo itakayotuwezesha kuzalisha chuma kingi hapa nchini kwa ajili ya viwanda vya ndani na  kuuza nje ya nchi sambamba na kurekebisha sheria na kanuni ili kuruhusu kuingizwa kwa urahisi malighafi zinazohitajika Katika uzalishaji wa bidhaa za vyuma "amesema Profesa Mkumbo 


Mwakilishi kutoka Tume ya Ushindani Allan Mlulla Kutoka Tume ya ushindani ambaye amehudhuria kikao hicho alisema Wam

echukua maelekezo yaliyotolewa na Waziri huku wakiahidi kuyafanyia kazi na kuchunguza huku atakayebainika kuchukuliwa hatua .


Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Sera na ushawishi shirikishi la Viwanda Akida Mnyenyelwa amesema kuwa kupitia kauli hiyo italeta tija kwa wafanyabiashara hapa nchini na wenye viwanda wataenda kuwekeza bila wasiwasi .


"Tumeongea na wazalishaji na wameshangaa kuona baadhi ya  vyombo vya Habari  vimeandika kwamba wazalishaji wa bidhaa viwandani wameongeza Bei kubwa .


 "Kama Waziri alivyoeleza hapo awali sababu za kuongezeka kidogo gharama na ni kutokana kwamba Kuna  ongezeko kidogo kwa ajili ya usambazaji  ambalo sio la kuleta taharuki kweny Jamii "alisema Mnyenyelwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post