MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA YAANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA LUCAS

 Na Mwandishi Wetu Mara.


Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Musoma Mkoani Mara imeanza kusikiliza kesi inayomkabili Mfanyabiashara anayefaamika kwa Jina la Lucas Sotel.


Lucas Sotel anakabiliwa na kesi ya mauaji ambayo ni kinyume cha sheria kifungu cha  1996 na 1997, kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 .


Mauji ya kijana Wankuru Nyamuhanga mkazi wa kijiji cha Buriba wiayani Tarime Mkoani Mara yanadaiwa kutendeka mnamo  Agosti 9 Mwaka 2014 katika kijiji cha Buriba.


Akiwasilisha shauri mbele ya jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Musoma iliyokaa wilayani Tarime  Mh: Jaji John Kahyoza  wakili wa serikali Yese Temba ameiambia mahakama kuwa katika shauri hilo kuna mashaidi wapatao watano.

Awali  wakili huyo aliiambia mahakama kuwa mashaidi tayari wamepewa wito wa mahakama ili  kuudhiria mahakama hiyo kwa ajili ya kutoa ushaidi juu ya mwenendo wa kesi hiyo lakini mpaka kesi inaanza kusikilizwa mashaidi  hawakuwepo mahakamani  hapo ndipo Mh: Jaji aliharisha kusilikiza kesi hiyo kwa muda.


Baada kuharisha kesi hiyo ilianza kusikilizwa tena kwa mara ya pili ambapo Mashaidi wawili kwa upande wa Jamhuri kati ya watatu ambao walipaswa kuwa mahakamani hapo walitoa ushaidi wao.


 Kati  ya Mashahidi hao shaidi mmoja ambaye alipewa wito na mahamama hiyo nakusaini wito nakushindwa kufika mahamamani hapo wakili wa srikali aliomba  mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa shaidi huyo ambapo  Mh Jaji mfawidhi Mahakama  kuu kanda ya Musoma Mh Jaji John Kahyoza aliagiza kukamatwa mara moja kwa  shahidi huyo ili aweze kutoa ushaidi.


Vilevile Jaji alisisitiza washauri wa mahakama kusaidia mahakama katika utoaji wa hukumu juu ya kesi hiyo na siyo kusikiliza ushaidi unatajwa mtaani bali wasikikiliza ushaidi unaotolewa mahakamani hapo.


 Mshitakiwa Lucas Sotel anatetewa na mawakili wawili ambayo ni Tumaini Kigombe Sayari na Selina Magoiga,  Wakili Kigombo wakati akiuliza maswali kwa mashaidi hao wote wawili katika mahakama mashaidi hayo walikili mbele ya mahakama kutomtambua mtu anayeyedaiwa kuua kijana Wankuru Nyamhanga ambaye kwa sasa ni Marehemu.


Baada ya kusikiliza ushaidi huo Mahakama haikuwa na maswali kwa  mashaidi hao ambapo Jaji Kahyoza  aliharisha kesi hiyo nakutajwa tena Novemba 29 mwaka huu.


             

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post