Wakristo watakiwa kutumaini Mungu

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wakristo wamekumbushwa kuwa moja ya wajibu wao ni kumtumainia Mungu kila wanapokutana  na changamoto mbalimbali kama sehemu ya utume wao, kwa kuwa vikwazo ni kipimo cha imani. 

Mafundisho hayo yametolewa na Mchungaji  wa kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga Charles Lugembe wakati akihubiri kwenye ibada maalum ya kumpongeza mratibu wa vijana dayosisi ya Shinyanga Benjamin Batano ambaye amestafu nafasi hiyo  aliyoitumikia kwa kipindi cha miaka 7

Mchungaji Lugembe amesema kila mkristo anapaswa kuwajibikia utume wake katika kukabiliana na vikwazo ama changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwani ndiyo ukamilifu wa kiimani 

“Vipo vikwazo vinapita pita lengo ni kukukwamisha ili ukwame kufikia mafanikio pamoja na mambo ambayo umeyalenga unapaswa kutambua wito wako kama mkristo na vikwazo vilivyopo ili kuwa na ushujaa wa kukabiliana navyo”

Mchungaji huyo ametaja baadhi ya vikwazo vinavyoweza kumkatisha tamaa mkristo kuwa ni pamoja na changamoto za kiichumi , kutengwa na ndugu, familia, kukosa kizazi pamoja na njaa, magonjwa kubaguliwa kutokana na hali na matatizo mengine ya aina kama hiyo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post