Watembelea gerezani na kutoa msaada kwa wafungwa

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Idara ya wanawake na watoto Pastokia ya Ngokolo leo wametembelea gereza la mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwasalimia wafungwa na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye gharama ya shilingi laki tatu.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa idara ya wanawake na watoto katika kanisa la AICT Ngokolo Rhoda Emmanueli amesema lengo la kwenda gerezani ni kupeleka neno la Mungu kwa kuwakumbusha pamoja na zawadi kwa wenye uhitaji wafungwa na mahabusu wa gereza hilo.

 

Ameziomba taasisi, makanisa, idara mbalimbali na jamii kujenga utaratibu wa kuwatembelea wafungwa kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo ili wasikate tamaa.

“Makanisa,taasisi na idara mbalimbali pamoja na jamii kwa ujumla ninawaomba tutafute njia na mpango wa kwenda kuwaona wenzetu walioko gerezani siyo kwamba wao ni wakosaji sana tunapoenda kuwaona tunawahamasisha  wasiendelee kutamani kukaa gerezani, wasitamani kurudi waachane na matendo maovu wamrudie Mungu”

Kwa upande wake mlezi na mshauri wa idara hiyo Tabitha Galani Makalanga amewaomba wakinamama kuwalea watoto katika maisha yanayo stahili pamoja na kuwaombea, ili wasifuate mambo ya dunia mbali waishi katika matendo yanayompendeza Mungu.

“Tuwalee watoto katika mazingira yanayostahili kwa sababu vijana ambao wanatakiwa wamsaidie mama lakini leo wanatumikia katika gereza wamama tunapokuwa na hali ya ujauzito tunapaswa kuomba kabla ya kujifungua wakati mwingine watoto hawa tunawalea katika mazingira yasiyompendeza Mungu tuwaombee ili waweze kuelewa kinachofanyika katika ulimwengu wanao ishi wasiishi kwa kufuata mambo ya kidunia waishi katika matendo yanayo mpendeza Mungu”amesema  Tabitha


Naye mkuu wa gereza la  Shinyanga Wiliam Makwaya amewashukuru wanawake wa idara hiyo kwa kuweza kuwakumbuka wafungwa hao ambapo amesema kwa yeyote atakaeguswa asisite kuwapelekea wafungwa na mahabusu waliopo katika gereza hilo 


Wakina mama wa kanisa la AICT Ngokolo wametoa msaada wa sabuni za B29, sabuni za kufuria za Jamaa na POA, mafuta ya kupaka makubwa na madogo, sabuni za unga, nguo za wananwake za wanaume,pamoja na vitabu vya biblia vya agano jipya.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post