Shinyanga wapewa magari mawili kukabiliana na mimba za utotoni

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali ya mkoa wa Shinyanga imepokea magari mawili kwa ajili ya kushughulikia ukatili kwa wanawake na mimba za utotoni  ili kupunguza na kuondoa kabisa ukatili katika mkoa wa Shinyanga 

Magari hayo yametolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu UNFPA kwa kushirikiana na shirika la United Nation Tanzania lengo kutoa elimu na kuwafikia wanaofanyiwa ukatili kwa uharaka

Katika makabidhiano hayo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh. Sophia Mjema amesema hatopenda kuona ukatili pamoja na mimba za utotoni zinaendelea katika mkoa wa Shinyanga ambapo amesema watashirikiana na viongozi wa dini na wazee wa mila ili kuondoa changamoto hizo

Mjema ameleelekeza katika kamati ya ulizi na usalama kwa wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga kuyatumia magari hayo kwa utaratibu na kufanya kazi iliyokusudiwa  ili kuhakikisha familia zinakuwa salama

“Magari haya tumepewa na wenzetu yakafanyekazi iliyokusudiwa sitakubali kuona siku nyingine gari linafanya kazi zingine kama siku hiyo kazi haipo gari lisitumiwe” amesema Mjema 

Mratibu wa shirika la umoja wa mataifa UNFPA kanda ya ziwa Dkt. Amir Batenga akiongozana na viongozi mbalimbali akiwemo  Jacqueline Mahona ambaye ni muwakarishi mkazi wa UNFPA Tanzania 

Batenga amesema mradi huo umeanza mwaka jana 2020 ambao umelenga kuwawezesha wanawake na watoto ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unaendelea 

Amesema iwapo magari hayo yatafanya kazi ambayo imekusudiwa katika kuwalinda wanawake na watoto ambapo waligundua kuwa changamoto kubwa inayosababisha kutowafikia walengwa kwa wakati ni usafiri 

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary amesema atahakikisha yeye pamoja na kamati yake  wanatekeleza sawa na makubaliano ili kuhakikisha mtoto wa kike na mwanamke wa Shinyanga analindwa

Kwa upande wake katibu wa kamati ya ulinzi na usalama wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale  amekili kuwepo kwa changamoto ya usafiri huku akisema watashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama  pamoja na taasisi mbalimbali kuhakikisha ukatili Mkoa wa Shinyanga unaisha

“Tumekuwa tabgu muda mrefu tunatumia magari yetu binafsi kuwakamata wahalifu, wabakaji na walio wapa mimba wananfunzi lakini kwa sasa tutaendelea kushirikiana na ofisi ya mwendesha mashtaka, mahakama, taasisi mbalimbali na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuushughulikia ukatili mkoa huu”

Magari hayo yamelenga kusaidia mkoa wa Shinyanga ambapo gari moja limeelekezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala ambapo ukatili  na mimba za utotoni zimeendelea kuwaathiri wasichana wengi katika eneo hilo lakini kwa sasa juhudi mbalimbali zinazoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA ili kuepuka mahusiano wasiyoyataka na yenye athari mbaya katika maisha yao

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango na kutoa ushirikiano  mkubwa kwa mashirika mbalimbali hasa ya kimataifa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post