Katambi aanza ziara ukaguzi miradi ya maendeleo Shinyanga

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia  kazi,vijana na ajira na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Paschal  Patrobas katambi ameanza ziara ya kikazi ya siku moja katika Jimbo lake kwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Katambi leo amekagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara katika kata ya Ibadakuli tawi la Uzogole, daraja la Chamaguha Kitangili, Masekelo na Ndala pamoja na kijiji cha Ihapa kata ya old shinyanga.

Mheshimiwa katambi ametahadharisha kuwa serikali haitawavumilia wakandarasi watakaotekeleza miradi chini ya kiwango kinachotakiwa 

“Kama mkandarasi tukikupa kazi iwe ya kutengeneza rami, madarasa au kutengeneza madaraja ukifanya chini ya kiwango hapa hautapata kazi ukija Shinyanga njoo umejipanga fedhi tutakazopewa kwenye mradi lazima tuangalie thamani ya fedha lakini pia tunategemea ufanye kazi vizuri”

Katambi amesema katika sekta ya michezo kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuwashinikiza  kuziinua timu za stend united pamoja na mwadui fc 

katambi amesema   hatua hiyo itakwenda sanjari na kufanyika kwa ligi ya mbunge ikiwa ni hatua ya  kuibua vipaji, kuimarisha afya   na kujenga mahusiano mema miongoni mwa wanajamii

mheshimiwa katambi amesema michezo hiyo itahusisha  makundi yote 

“Kwenye sekta ya michezo nipo kwenye mazungumzo na kampuni mbalimbali kuweza kuangalia ni namna gani tutawainua vijana wa Shinyanga wapo wachezaji wazuri na wanakipaji na uwezo mkubwa lakini tutaanza sambaba na kuanza ligi ya mbunge ambapo waheshimiwa madiwani wataanzisha mashindano kwenye kata timu bora zitaingia kwenye lingi ya jimbo”

Katambi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki na kuchangia nguvu kwenye shughuli za utekelezaji wa miradi ya kijamii ili kuleta maendeleo

“Niwahamazishe wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini na niwaombe tunapokuwa na shughuli za maendeleo wajitokeze kwa wingi ili tuweze kushiriki kwa pamoja’ 

Katika ziara hiyo wananchi wamemshukuru na kumpongeza mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Paschal  Patrobas Katambi kwa kusimamia na kuweka msukumo wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara, madaraja na karavati.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post