Mmanywa aapishwa, aanza rasmi kutumikia wananchi wa Ndembezi

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Diwani mpya wa kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga Victor Thobias Mmanywa leo ameapishwa rasmi kupitia kikao cha kawaida cha baraza la diwani ambacho kimenza leo Jumamosi ikiwa ni hatua ya kuanza utekelezaji wa majukumu yake.

Mmanywa anakuwa diwani mpya wa kata ya Ndemezi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo hayati David Nkulila ambaye amefariki dunia wiki chache zilizopita.

Akizungumza baada ya kumkabidhi kitabu cha sheria na kanuni za maadili ya utumishi wa umma katibu msaidizi ofisi ya rais,Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma katika kanda ya Magharibi Gelard Mwaitebele amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kila mmoja wake kutatua kero za wananchi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu wanapofanya ziara.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko maetumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kwa kushirikiana na wataalam kusimamia kikamilifu fedha ambazo zinatolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kuwashirikisha wananchi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post