Watakiwa kutumia saccos kujiinua kiuchumi

Beda Kamara

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Watumishi wa umma katika mkoa wa Shinyanga wameshauriwa kuwa wabunifu ili kujiinua kiuchumi kupitia chama chao cha kuweka na kukopa cha Kurugenzi SACCOS.

Wito huo umetolewa na katibu tawala msaidizi, utawala na raslimali watu  wa mkoa wa Shinyanga Beda Kamara wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho.

“Lakini tufikirie kurugenzi SACCOS ambayo inaendana na na Sayansi na Teknolojia ya kisasa tufikirie kwenda kwenye tehama kwenye mfumo rahisi na uwepesi wa mawasiliano na wanachama pamoja na shughuli zote za uendeshaji wa chama”

Bwana kamara ambaye alikuwa amemwakilisha katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omar ,pia amewataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanafuatilia mwenendo wa urejeshaji wa fedha kwa wanachama ili kikundi hicho kiweze kuendelea.

“Kunahaja ya kuangalia mwenendo wa mwanachama mmoja mmoja hasa mwenendo wa kitabia, ukopaji na urejeshaji wapo wananchama wanakwamisha anamkopo lakini marejesho ni duni, hafifu au hakuna kabisa”amesema Kamara 


Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya Kurugenzi SACCOSS Marwa Kisibo ameahidi kwenda kushugulikia changamoto zilizopo huku akiwataka baadhi ya wanachama ambao hawarejeshi mikopo ya kwa wakati wabadilike

“Changamoto kubwa za chama zinatokana na madeni na madeni hayo yanasababishwa na wanachama kwahiyo niwatake wawe waaminifu pale wanapochukua mikopo wairejeshe kwa mudu tuliokubaliana ili chama kiwe na nguvu ya fedha na kinamuwezesha mwanachama kukopa tena na tena hatimaye kujenga uchumi na kutatua changamoto za maisha”

Kurugenzi SACCOS ambayo imeanzishwa mwaka 1978 ni chama cha kuweka na kukopa ambacho kinajumuisha watumishi wa umma kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga,Ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga mamlaka ya maji na wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post