Watoto waiba meza 30 na viti50 mali ya sekondari ya Ibinzamata

 Na  Mapuli  Misalaba, Shinyanga


Watoto Wanne  wenye umri kati ya Miaka 14 hadi 16 akiwemo Mwanafunzi mmoja wamefikishwa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, wakituhumiwa kuiba meza 30 na viti 50 mali ya shule ya Sekondari Ibinzamata


Afisa mtendaji wa kata hiyo VICTOR

KAJUNA amekiri watoto hao kufikishwa katika ofisi yake wakituhumiwa kuhusika  na wizi wa samani hizo katika shule ya Sekondari Ibinzamata,na kwamba kutokana na mahojiano na vijana hao imebainika kuwa vitendo vya uhalifu ni tabia yao


“Lakini kwenye mahojiano wamesema siyo mara yao ya kwanza kuiba na siyo eneo moja ikiwemo shule ya msingi buhangija wameiba koki za maji 8, madawati 12 lakini pia kuna chuo cha maendeleo ya wananchi FDC waliiba mishikio ya masufulia mawili wakaenda kuuza”amesema Kajuna


Mtendaji huyo amesema vijana hao wamekiri kuhusika na wizi wa samani hizo  ambazo wamekuwa wakivivunja ili kuchukua vyuma na kuviuza kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu Mjini Shinyanga,ili kujipatia kipato kwa ajili ya kwenda kucheza michezo jamii ya kamali


“Wamekiri wanamuda mrefu wakifanya haya matukio lakini kinachopelekea ni michezo ya pool pamoja na Bonanza kwamba hiyo ni michezo inatumia pesa kwahiyo wakikosa pesa ndo wanaenda kuiba kwa wafanyabiashara ya pool tumeshawapa utaratibu watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kucheza pool lakini pia na muda wa kuanza saa kumi mpaka saa nne usiku na ni watu wazima tu”


Watoto hao ni Paschal Boniphance mwenye umri wa miaka (14)’ Jolam Danifodi(16), Frenck Simon (16) anasoma darasa la sita, Masa Abazi (14)


Mkuu wa shule ya sekondari Ibinzamata  Mwalimu Richard kisandu amesema tukio la wizi limetokea Septemba 18,Mwaka huu na kwamba vijana hao wamekamatwa leo ambapo baada ya Uchunguzi kufanyika  vyuma vilivyobanduliwa kwenye samani hizo vilipatikana  akiwa ameuziwa mfanyabiashara mmoja  wa vyuma chakavu ambaye alitakiwa kulipa faini ya shilingi laki nane,huku wazazi wa watoto watalipa gharama ya samani zote hizo  


“Baada ya kuchunguza kufanyika kwa kushirikiana na uongozi wa kta pamoja na sungusungu Bugayambelele tulivipata vyuma hivi vikiwa tayari vimenunuliwa tumechukua hatua ya kuwatafuta wazazi wao pamoja na mnunuzi adhabu iliyotolewa kwa kwanza kuhakikisha zile meza na viti zinatengenezwa zote lakini mnunuzi amelipa faini ya shilingi laki nane na tayari ameshaingiza kwenye akaunti ya shule”


Kisandu ametoa wito kwa wazazi kuwalea watoto katika mazingira rafiki “Kwa taarifa hii natoa rai kwa wazazi kuwalea watoto wao katika mazingira rafiki badala kujishirikisha katika makundi mabaya na iwe fundisho kwa watoto wetu kwamba vitendo hivi vinarudisha nyuma maendeleo ya shule pamoja na Taifa kwa ujumla”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post