Watoa msaada wa mitungi ya gesi kuokoa wagonjwa wa Uviko

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Jukwaa la mitandao ya kijamii Whats-sap lijulikanalo kwa jina la “OKOA UHAI NUNUA MITUNGI”  limetoa msaada wa mitungi 10 ya hewa ya Oksijeni kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wa Uviko 19 wanaopata changamoto ya upumuaji katika Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga


Akikabidhi mitungi hiyo mratibu wa kikundi hicho GWAKISA MWASYEBA amesema aliamua  kuanzisha kikundi cha wasap ili kusaidia kununua mitungi ya Oksijeni ambayo thamani yake ni shilingi 695,000


Amesema kundi hilo la wasap linajumla ya wanachama 83 kati ya hao wanachama 21 waliweza kutoa mchango kwa upendo na uaminifu ndani ya mwezi mmoja na nusu 


“Kipindi cha mwezi Julai kulitokea upungufu kidogo wa mitungi ya gesi ya Oksijeni kwa ajili ya wagojwa wa Uviko 19 hivyo kutokana na upendo tulionao watanzania nikaanzisha kundi (group) la wasapu  kwa ajili ya kusaidia kununua mitungi ya Oksijeni kwa muda mfupi wanakikundi waliunga wazo nikapata wajumbe sehemu mbalimbali ya Tanzania Bara. Kundi hili la wasapu linawajumbe 83 kati ya hao wajumbe 21 waliweza kutoa mchango na ahadi kufikia tarehe 22 mwezi wa 09, 2021 kiasi cha shilingi 695,000 kimekusanywa kutoka kwa wanakikundi”


Akizungumza katika hafla ya kupokea mitungi hiyo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga JASINTA MBONEKO amekipongeza kikundi hicho na kuvitaka  vikundi vingine  kuiga mfano huo wa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kueneza upendo na kudumisha amani kwa kusaidia watu pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuisaidia jamii, kuwajali wagonjwa na wenye uhitaji 


“Nitoe rai kwa wasap groups zingine zilizopo kwenye wilaya yetu na maeneo mengine kuyatumia magroup haya kwa kusaidia watu lakini kwa kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo maana kunavikundi wapo watu zaidi ya miambili lakini kuanzia Januari mpaka Desemba ni kusogoa tu,maneno tu,picha tu hakuna jambo ambalo wao wamelifanya kwenye jamii. Kwahiyo nitoe rai tena kwa wanakikundi wengine hata mkiwa wanagroup 200 mkichanga elfu moja moja tu mnanunua mifuko ya Simenti mnasema tunapeleka kwa ajili ya kujenga choo, kutengeneza darasa inawezekana sisi serikali tunapokea kwahiyo maendeleo yanafanywa na wananchi kusaidiana na serikali yao ni muhimu kuijari jamii, kujari wanaoumwa na kuwasaidia wahitaji”


Kwa upande wake  kaimu mganga mfawidhi wa Hospatal ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga RICHARD MUHANGWA amesema mitungi hiyo itasaidia sana kwa wagonjwa na itarahisisha utoaji wa huduma 


“Kwa hawa group la wasap tunaendelea kutoa shukurani zetu za dhati mitungi 10 ni msaada mkubwa sana kwanza itaturahisishia sisi katika utoaji wa huduma nadhani watumishiwenzangu ni mashahidi changamoto ambazo tulikuwa tunazipata hasa kwa wagonjwa wenye uhitaji wa Oksijeni niwashukuru sana hasa mratibu ambaye aliweza kufikiria hii njia ni wazo zuri ambalo tumeona chanya ya matumizi ya ya mitandao ya kijamii”


Aidha kaimu mganga mfawidhi wa Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga amesema takwimu ya wagonjwa wa Uviko 19 katika Hospital hiyo waliopo kwa sasa 5 kati ya hao  mwenye uhitaji ni mmoja.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post