Kuelekea msimu wa mvua,wananchi Shinyanga Watakiwa kuzingatia usafi

 Na  Mapuli Misalaba,  Shinyanga

Idara ya Afya katika Halmashari ya Manispaa ya Shinyanga imewataka Wananchi wote kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kufanya usafi katika makazi yao,kudhibiti utupaji wa taka ovyo, pamoja na kuwa na vyoo Bora na imara.

Ramadhan Hamim, afsa Afya Manispaa ya Shinyanga

Wito huo umetolewa na Mratibu wa  afya Manispaa ya Shinyanga Bwana Ramadhan Hamimu wakati alipotembelea kata ya Ibinzamata kuhamasisha suala la usafi wa mazingira ambapo amesema Halmashauri hiyo itasimamia na kuhakikisha kila mwananchi anafanya usafi katika makazi yake,ikiwa ni pamoja na  kudhibiti utupaji wa taka ovyo. 

Amesema Idara ya afya kwa kutumia sheria na kanuzi za usafi wa mazingira itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukaidi utekelezaji wa agizo hilo muhimu ambalo limelenga kuweka mazingira yote katika hali ya usafi.

“Kuna mtu anafagia halafu taka anatupa kwenye kiwanja cha mtu mwingine yaani hana sehemu yake ya kuhifadhia taka ukitupa taka kwenye kiwanja siyo chakwako hilo ni kosa la jinai kisheria na ndiyo maana kisheria kama kiwanja cha jirani yako kipo wazi unatakiwa ukisafishe nikikuta kichafu kinamakaratasi nakukamata wewe kwa sababu yeye hayupo hapo kimechafukaje”

Amesisitiza umuhimu wa kila Mwananchi kuwa na Choo bora na imara hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye msimu wa Mvua za Masika ili kudhibiti maonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, na kuhara.

“Vyoo tunavyo lakini havina sifa ya kuwa vyoo yaani tumejiwekea sehemu ya kujificha tu lakini siyo vile vyoo ambavyo vinahitajika hapa Manispaa ya Shinyanga kwanza tunaingia msimu wa mvua jana nimetembelea kaya zaidi ya miamoja lakini nimekuta kaya angalau vimeezeka tu ni kaya 23 kaya zingine zote vyoo vyao vikowazi kwa juu,"

Amesema na kuongeza" msimu wa mvua unaingia badae  vyoo vyote vitakuja kutitia ukimfuata mtu anakwambia huu ni msimu wa mvua kimetitia, na mimi sitokuelewa kabisa nataka choo chako nikikute kimeezekwa na kina mlango hiyo ni lazima kwa hiyo mimi sitaki tufike huko ustaarabu ni kusafisha mazingira, hakuna kutupa taka ovyo nikikuta taka zimezagaa kwako hilo ni kosa,".

Alisema yoyote atakayekamatwa na kosa la uchafunzi wa mazingira atapigwa faini ya Shilingi elfu hamsini(50000) na kwamba hawatishi hiyo ni kwa mujibu wa sheria.

"Nipo kwa ajili ya kulinda afya zenu ili msipate magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu, kuhara na magonjwa mengine”aliongeza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post