NI ZAIDI YA UPENDO, WALICHOKIFANYA "KIVULE MAENDELEO KWANZA", MISAADA KWA WAJANE YATOLEWA

  Na Mwandishi Wetu.

Jukwaa la kimaendeleo la Kivule Maendeleo Kwanza, limefanya tafrija ya kuungana na waislam katika mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kufuturisha Watu wa kivule na wageni waalikwa, huku mgeni rasmi akiwa Katibu wa  Mbunge wa Jimbo la Ukonga Alphonce Msibuko ambaye alimuwakilisha Mbunge wa Ukonga Ndugu Jerry Slaa.Akiongea katika hafra hiyo, Ndugu Msimbo, amesema kuwa, kitendo walichokifanya Jukwaa la Kivule Maendeleo Kwanza ni kitendo cha kuigwa, maana kunamatatizo yanatakiwa kutatuliwa na wananchi kwakushirikiana kama wanavyofanya wanajukwaa hilo, kwakuwa si kila tatizo litatatuliwa na serikali kuu."Mheshimiwa Mbunge amenituma nije nimuwakilishe, kwakuwa kama mnavyojua kipindi hiki ni cha bunge la bajeti, hivyo wabunge wako kuhakikisha wanawasilisha mambo ya majimbo yao, pamoja na kufanya ushawishi wa karibu kwa viongozi mbalimbali, hivyo ameshindwa kufika, ingawa alitamani sana kushiriki nanyi katika tukio hili"
"Risala hii, Mimi nimeichukua, na kama mwakilishi, Mheshimiwa mbunge ataipata, uzuri kunateknolojia sikiuhizi. Lakini pia Mheshimia ameahidi akitoka huko atapitia kata kwa kata kusikiliza kero zaidi na kupata fursa ya kuwashukuru kwa kumpa kura. Na amesema ataona namna atapambana kwakushirikiana na Madiwani kutatua kero, kwa zile zilizo ndani ya uwezo wake zitatatuliwa na zile zinazoihusu serikali zitawasilishwa na kutiliwa mkazo ili zitatuliwe"
Kwa upande wake kiongozi wa waanzilishi wa Jukwaa hilo, Ndugu Bihimba Nasoro amesema kuwa lengo kuu la kuanzisha jukwaa hilo lilikuwa ni kuwaleta pamoja Wanakivule, ili kujadiliana mambo ya maendeleo ya Kata yao kiujumla ili kuwa na sauti ya pamoja ya upazaji sauti za kero zao. Anasema waliona ni ngumu kila mmoja kufika kwa kiongizi kuwasilisha kero yake au anayoiona.


Aliongeza kuwa, wao lengo lao kuu ni kuona kero za Kivule zinatatulika kwa ushiriki wa Wananchi na pia kwakuwashirikisha viongozi kwa zile zinazopaswa kutatuliwa na viongozi.


Alisema changamoto ni nyingi, ingawa tangu waanzishe jukwaa hilo wamefanikiwa kutatua kero nyingi ikiwemo kushiriki katika kurekebisha miundombinu ya barabara, kushiriki katika masuala ya kijamii, kusaidia wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kutia motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na walimu wa shule za Kivule.
Akisoma risala yao, Miongoni mwa waanzilishi wa jukwa hilo, Ndugu. V.E Banda, amesema, jukwa hilo limefanikiwa kuwaunganisha Wanakivule, kushiriki katika shughuli za kijamii, ikiwa ni pamoja na kukusanya kiasi cha milioni 11.3 zilizotumika kutatua changamoto mbalimbali kwa Wanakivule zaidi ya 37. Amesema, tukio la kuandaa futari kwaajiri ya wanakivule waliokatika mfungo wa ramadhani na wageni waalikwa ni moja ya mafanikio pia kwakuwa limewaleta pamoja wadau mbalimbali ikiwemo wamiliki wa mashule, vituo vya afya, ili kuwahamasisha nao kushiriki katika kutatua changamoto za jamii.

Banda ameongeza kuwa, pamoja na mafanikio hao, kunachangamoto zinawakabili, kama vile ushiriki hafifu kwa baadhi ya wanajukwaa, pamoja na mwitikio hafifu kwa viongozi katika kutatua kero wanazoziwasilisha, ikiwemo ya barabara, madaraja na ufaulu mdogo wa wanafunzi wa sekondari.


Walimuomba Mbunge kuwatembelea na kufanya mikutano ya mara kwa mara ili kufahamu kwa ukaribu changamoto zao.
Tafrija hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya mstaafu, Mama Msangi, ambaye alitoa msaada kwa mama wajane wa Kivule. Amesema kuwa yeye katika umri alioubakiza hapa duniani, amejidhatiti katika kushiriki kutatua changamoto za wananchi hasa kwaakina Mama na Wasichana ili kuwa na Wakinamama bora wa baadaye.


"Ni wachache ambao wameweza kutimiza tendo kama hili la kuwaweka watu pamoja kama hivi. Nawapongeza kwakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa ngazi ya chini ya kata. Nimejifunza mengi sana na changamoto nyingi sana, lakini changamoto sio tatizo, tatizo ni pale unapoikimbia changamoto" 
"Nimejaaliwa kuleta sadaka kidogo sana, lakini kubwa sana katika sadaka ni kuguswa moyoni, na mimi ameguswa na wanakivule. Jambo lingine nililoguswa ni ufaulu wa shule zetu si mzuri sana. Kwa mda aliobakia ingawa ni mchache, lakini nitasaidia kwenye taaluma yangu hii ya elimu, ingawa nakumbana na changamoto ya fedha lakini nimeshaanza na nimepata eneo""Na nyie akinamama wajane, msikae kihuzuni. Ujane siougonjwa, ni hali wanayoipitia watu wengi, akina mama na akinababa pia. Kwahiyo sio kusononeka, ni kumshukuru Mwenyezi Mungu na kubaki mnajiuliza tufanye nini. Inatakiwa kujikaza mkanda, tukae pamoja tujue namna ya kujiletea maendeleo"


Wageni wengine waliohudhuria kama wageni waalikwa ni Mchungaji wa kanisa la Wasabato, Mchungaji Mmole Mtokambali, Diwani wa Ukonga, Mwansheria wa Jiji la Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali za mtaa.

Wageni wote walipongeza hatua ya jukwaa hilo na kusisitiza kuliendeleza na kulitumia kuleta umoja, mshikamano na kujadiliana vyema juu ya maendeleo ya kivule na nchi kwa ujumla bila kubaguana kiimani, siasa wala nafasi zao katika jamii.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post