Wazazi watakiwa kuwekeza kwa watoto

 

 mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro katikati akiwa  pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB mara baada ya kuzindua  rasmi akaunti ya mtoto ijulikanayo kama Junior Jumbo Account
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Jelly Murro   akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CRDB ,wazazi na watoto juzi  mara baada ya kuzindua rasmi   account ya mtoto ijulikanayo kama [Junior Jumbo account] kutoka CRDBNa Woinde Shizza ,ARUSHA

 

Malezi bora katika familia ndiyo msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wametakiwa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto wao ndani ya familia na jamii kwa jumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

 

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jelly Murro  wakati akizindua account ya mtoto ijulikanayo kama [Junior Jumbo account] kutoka CRDB  ambapo alisema  wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na wawe na utaratibu wa kuwawekea akiba ya pesa kwa ajili ya maisha yao  ya badae ili iweze kuwasaidia katika masomo yao na itawajengea  maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, kujithamini.

 

Muro alisema wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu, uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.

 

“unapo muwekea mtoto akiba yake katika benki kwanza inakusaidia wewe mzazi kuwa na uhakikia wa kulipa ada kwa muda wowote pia ,mnajua kabisa wazazi mtoto unaporudishwa rudishwa ada unamuathiri kisaikolojia kwani atapata mawazo mengi ambayo yatampelekea hata kushidwa kufanya vizuri darasani”alisema Muro

  

Kwa upande wake Neema  Njau ambae ni mzazi alisema kuwawekea watoto na vijana akiba ni utaratibu mzuri wa kuweza kuwasadia katika kujiendeleza kielimu na kujenga taifa lenye maadili na upendo.

 

 

 Kwa upande wake meneja biashara wa kanda David Peter  alisema kuwa wanatambua wateja wao wana malengo ambayo wamejiwekea katika maisha yao, na wao kama Benki ya kizalendo wana jukumu la kuhakikisha wateja  wanafikia malengo yao kupitia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki  ikiwemo huduma ya kuweka akiba kupitia akaunti mbalimbali kama vile akaunti hii ya Junior Jumbo account.

 

 

Alisema wanaendelea kuboresha huduma na miundombinu yake ya kutoa huduma hususani ile ya kidijitali, ambapo aliwataka wateja kuwafungulia watoto wao akaunti hii  kwani ni mkombozi mkubwa sana kwa mtoto   na nimsaada mkubwa pia kwa mzazi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post