TAKUKURU ILALA YAOKOA MABILIONI YA SHILINGI

TAASISI ya Kuzuia  Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa ilala imeokoa na Kudhibiti fedha kiasi cha shilingi Billioni 1,037,207,090 zikiwa ni fedha za mfuko wa Taifa wa Pembejeo( AGITF) na mfuko wa huduma wa Hifadhi ya jamii(PSSSF).

Kauli hiyo imeitolewa  mapema leo jijini Dar es salaam na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ilala Christopher Myava wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa umma katika kipindi cha kila robo mwaka Januari hadi Machi.

Ameongeza kuwa, mfuko wa Taifa wa Pembejeo ulitoa fedha kwenye benki mbalimbali ili wazikopeshe kwa wakulima lakini fedha hizo hazikurudishwa katika mfuko huo hata baada ya wakulima kuzirudisha fedha hizo kwenye benki walizokopa.

Amesema kuwa, kitendo hicho kinatafsiriwa kama cha kujinufaisha kwa kutumia fedha za Serikali kinyume na sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, ambapo mpaka Sasa fedha zilizorejeshwa kwa miezi mitatu ni shilingi millioni 688,278,090.


"mfuko wa huduma wa Hifadhi ya jamii(PSSSF) walizikopesha SACCOS za Taasisi mbalimbali ili wakopeshe kwa Wanachama wao badae wazirejeshe PSSSF lakini hazikurejeshwa ambapo kiasi kilichorejeshwa kwa kipindu cha miezi mitatu ni shilingi millioni 348,909,000 na fedha ambazo hazijarurushwa tutaendelea kuzifatilia ili zirejeshwe serikalini" amesema  Myava


Hata hivyo, amesema katika kipindi cha  Januari hadi Machi 2021 TAKUKURU mkoa wa ilala imefungua kesi mpya 4 na mashauri  22 yanaendelea mahakamani.


Ameongeza kuwa, mashauri hayo yalioko mahakamani ni pamoja na shauri la Mamlaka ya Mapato (TRA)4, Serikali za mitaa mashauri 4, wafanyabishara 3, Idala ya Afya 3,ujenzi 2, Elimu ya juu 1,Ardhi 1, Vyama vya Siasa 2, Maji 1 na Aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU 1.


Katika hatua nyingine amesema TAKUKURU mkoa wa ilala imepokea taarifa 303 ambapo katika taarifa hizo malalamiko yalihusu Rushwa ni 102, huku idara zinazolalamikiwa zikiwa 32 ni za serikali ya mitaa ,mahakama 25, Polisi 20 na Afya 06.


Amesema kuwa, uchunguzi wa taarifa hizo na zingine unaendelea katika hatua mbalimbali

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post