Mdee aivimbia Chadema: Hatuondoki, ' tumekuzwa chadema', tutapambana hadi hatua ya mwisho

 Na Mwandishi Wetu, 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amesema yeye, pamoja na wenzake 18 hawatoondoka ndani a chama hicho na wanaendelea na utaratibu wa kuakta rufaa kupinga maamuzi ya wao kufukuzwa.

Akizungumza leo Jumanne Disemba 1, 2020 Jijini Dar es salaam katika kikao chake na vyombo vya habari, ambapo pia aliambatana na wabunge wengine 18 waliofukuzwa uanachama na chama hicho baada ya kukubalia kuapishwa kama wabunge wa viti maalum, mdee amesema.

"Uamuzi wa kamati kuu, ulitolewa mbele ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe tarehe 27 Novemba 2020 akisema, Mdee na wenzake wamekisaliti chama na kama hawaridhiki na uamuzi huo, wanaweza kukata rufaa baraza kuu ndani ya siku 30 au kuomba radhi.

akizungumza mbele ya wanahabari amesema ' mimi na wenzangu tutakuwa wana Chadema Kinga'ng'anizi  na ndiyo maana tumepiga kombati. Yaani unakataliwa lakini unang'ang'ania".

Mdee amesema, yenye pamoja na wenzake wanatambua mchango mkubwa wa  Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Mbowe "Kwangu mimi binafsi, huwezi kumzungumzia Halima bila kumtaja Mbowe na wenzangu kwa nafasi zao. Tunamheshimu sana Mbowe,".

" Mimi na wenzangu tumechukuliwa hatua na kamati kuu, niwahakikishie , mimi na wenzangu tutabaki kuwa wana Chadema kindakindani . Mimi dhamira ya kuondoka Chadema haipo. Pamoja na changamoto ya kisiasa tunayoipitia , Halima mnayemfahamu miaka yote, ni yule yule na nikisema Halima na timu yangu yote,"amesema.

"Kati ya wanawake 19 na 15 waliogombea kwenye majimbo na walifanya vizuri sana na kama uchaguzi usingekuwa na sintofahamu nyingi kama kwangu Kawe, wote tungekwenda mjengoni,"amesema.

aidha mdee anasema " mimi ni mhanga kweli kweli wa siasa za mageuzi, nitakuwa mwendawazimu jana nimesema uchaguzi ulikuwa hivi, halafu nije nikubaliane na haya. Haya tunayopitia ni changamoto za kisiasa tu."

"wanasema Mdee na wenzake, mimi  nakubali kupigwa mawe yote. lakini  niwahikishie wana chadema, kama nimepewa hela na rushwa  haina siri  na hakuna yoyote na kama kuna mambo yalitokea, yalikuwa na dhamira njemba kabisa," amesema.

"Mimi Halima Mdee sijawahi kununuliwa, na sitanunuliwa na sitarajii kununuliwa. Watu wanaofanya kazi na mimi iwe kwenye chama kwa miaka 16 iwe bungeni kwa miaka 15, wanajua taja watu watatu ambao rushwa kwao ni mwiko, nawezekana nikawa wa kwanza," amesema.

Mdee amesema , yeye pamoaj na wenzake, "hatuondoki Chadema, tutaendelea na taratibu za ndani na kuzimaliza. tutaendelea kuwa wana Chadema wa hiyari na tutaendelea na taratibu za kukata rufaa. Katika mapambano ya siasa, huwezi kuacha kumtaja (Freeman Mbowe)".

Mbali na Mdee kufukuzwa wengien ni waliokuwa wajumbe wa kamati kuu ya Chadema, Ester Matiko, na Ester Bulaya, Katibu Mkuu wa Bavicha Nusrat Hanje, Katibu Mkuu Baraza la wanawake Chadema, Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga, Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa na Katibu Mwenezi Bawacha     Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mtwara Tunza Malapo, Cecilia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post