SIDA na harakati zake za kunusuru waandishi wa habari dhidi ya ugonjwa wa Corona

 

Na Mustafa  Leu. 

ULIMWENGU upo katika taharuki  kubwa inayotokana na kukumbwa na ugonjwa wa mlipuko wa Covid-19 ambao mpaka sasa hauna tiba wala kinga na umesababisha  maelfu ya watu kufariki dunia .

Wataalam wa afya wanaendelea kukesha kwenye maabara kutafuta dawa na tiba sahihi ya ugonjwa huu wa Covid-19 ambao haujafahamika chanzo chake mbali ya kuwa na madhara makubwa ikiwemo vifo na kuporopmoka kwa uchumi.

Baada ya kulipuka kwa ugonjwa huo kila nchi imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana nao kwa lengo la kuutokomeza na kuwakinga wananchi wake wasipate maambukizi na kuathiri uzalishaji.

Miongoni mwa hatua za awali zilizochukuliwa hapa nchini kwetu ni pamoja na Serikali kushauri viongozi wa dini kuhakikisha wanaendesha ibada maalumu kwa waumini wake kwa kumuomba Mungu kutuepusha na janga hilo, hamasa ambayo iliwashirikisha hadi viongozi wa mila.

Tuna kila sababu ya kumshukuru mungu, kwa kutunusuru na maambukizi hayo ya ugonjwa huo wa Covid-19 na sasa tupo salama,lakini wakati sie tupo salama zipo nchi zinazotuzunguka bado zina kabiliwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Ongezeko hilo la maambukizi linazifanya nchi hizo kukuna vichwa ni namna gani wataepukana na maambukizi kwa kuwa kila siku taarifa zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi bado kinaongezeka hivyo nchi hizo zinaendelea kuchukua hatua kwa kuweka masharti kwa wananchi wake ili waweze kujikinga na maambukizi .

Afisa Programu wa UTPC Victor Maleko akizungumza na wanachama wa Arusha Press Club wakati wa mafunzo kuhusu magonjwa ya mlipuko yaliyofanyika hivi karibuni Arusha, wa pili kulia kwake ni Claud Gwandu Mwenyekiti wa APC na wa kwanza kushoto kwake ni Mussa Juma Makamu Mwenyekiti wa APC

.Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari Arusha wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa mafunzo kuhusu magonjwa ya kuambukiza Dkt Francis David (hayupo pichani), mafunzo hayo yalidhaminiwa na UTPC.

Mbali na Viongozi wa dini kuendesha Ibada maalumu, pia serikali ilihamasisha matumizi ya dawa za asili zikiwemo za kujifukiza, kuhamasisha matumizi ya viungo mbalimbali kama tangawizi, limao, na ulaji wa matunda kwa wingi .

Pia ilitolewa hamasa kwa wananchi kusikiliza ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu hatua za kujikinga na maambukizi hayo ya ugonjwa huo wa Covid -19.

Pia kulitengwa maeneo maalumu ya kuhudumia watu watakaokuwa wamepata maambukizi ya ugonjwa huo ili wasiusambaze na kuenea kwa watu wengi zaidi.

Katika kuhakikisha ugonjwa huo hauenei ,Ulimwengu ulisitisha safari zote zikiwemo za ndege,meli, treni,magari,kutoka nchi moja kwenda nyingine,kuweka vizuizi au karantini wagonjwa wa Covid-19.

Wakati wa kutekeleza hatua hizo uchumi ulimwenguni umeporomoka ambapo shughuli za uzalishaji wa  bidhaa ikiwemo utalii  zilishuka kwa kiwango kikubwa sana na hata kupunguzwa kwa wafanyakazi kwenye maeneo mbalimbali .

Kutokana na ulimwengu kukumbwa na maambukizi hayo Shirika la misaada la Sweden, SIDA, linajitokeza kuendesha mafunzo ya kuwakinga wanahabari dhidi ya  maambukizi hayo ya ugonjwa huo wa Covid-19.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwawawezesha wanahabari kujikinga na kuwa na tahadhari dhidi ya  kupata maambukizi hayo kutokana na wao kuwa ni miongoni mwa jamii inayoweza kuambukizwa kwa haraka kutokana na kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi.

Sida, imefadhili  mafunzo hayo kupitia mradi wake unaosimamiwa na Umoja wa vilabu vya wanahabari nchini UTPC, ili kuwaokoa wanahabari wasiambukizwe ugonjwa huo ambao hauna kinga wala tiba.

Mafunzo hayo yanatolewa kutokana na kutambua umuhimu mkubwa wa wanahabari kuwa ni kundi ambalo lipo katika hatari kubwa ya kukumbwa na ugonjwa huo.

 Pia Wanahabari ni kundi muhimu katika maendeleo ya nchi kutokana na unyeti wa kazi zao wanazozifanya za kuelimisha na kuhabarisha umma.

Kutokana na wanahabari kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi hayo kutokana na kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi Shirika hilo la Sida,likaona ni muhimu kutoa mafunzo ya kuwakinga wanahabari nchini dhidi ya  maambukizi ya ugonjwa huo wa mlipuko wa Covid -19.

Katika kuhakikisha wanahabari wanapewa dozi ya mafunzo ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo UTPC ilitoa mwongozo kuwa klabu za waandishi wa habari kutafuta wataalamu wa afya kutoa mafunzo hayo kwa wanahabari kutokana na uzoefu wao wa namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko .

Mafunzo hayo yanajikita kuwaokoa wanahabari ili wasipate maambukizi ya ugonjwa huo,na hivyo kuwawezesha kuendelea na majukumu yao wakiwa salama.

Hongera sana SIDA,kwa kuliona hilo la umuhimu wa mafunzo kwa wanahabari kwa kuwa wanahabari wakiambukizwa ugonjwa huo wa mlipuko umma utakosa taarifa na hivyo nchi itaangamia.

Kwa kipindi kirefu SIDA imekuwa ni nguzo na muhimili mkubwa wa sekta ya habari nchini imekuwa ikifadhili mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuwanoa kwenye taaluma ili wawe ni mahiri .

Afisa Programu wa UTPC,Victor Maleko akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo anasema kuwa mafunzo hayo yanayoambatana na kutolewa vifaa vya kujikinga yanawezesha wanahabari kuepuka maambukizi.

Anasema mafunzo hayo ni muhimu sana kuliko kitu kingine chochote kwa mwanahabari kwa kuwa wao ndio tegemeo la wananchi kupata taarifa za maambukizi na hatua za kujikinga.

Kwa upande wake Daktari Francis David, kutoka hospitali ya Aghakhan tawi la Arusha ,akiendesha mafunzo hayo anasema kuwa  ni muhimu kwa wanahabari kupewa elimu hiyo kutokana na umuhimu wao kwa kuwa umma.

Anasema Umma,unawategemea wanahabari  kupata taarifa kuhusu kiwango cha maambukizi na hatua za kuchukua kujikinga na maambukizi hayo ya ugonjwa huo wa mlipuko.

Anasema kirusi hicho cha Covid-19 kina weza kuishi kwenye sehemu yeyote kwa muda wa saa 8 kutoka kwa mtu aliyeambukizwa mara baada ya kupiga chafya kwa kuwa kinakuwa bado kipo kwenye mazingira ya majimaji.

Kirusi hicho ambacho huambukiza  kwa njia ya hewa ,kugusa maeneo ya wazi ambayo ni pua,macho na mdomo ambapo kirusi kikishaingia mwilini na kukaa kwenye koo na kisha kuingia ndani ya mwili .

Anasema kikisha kaa ndani ya mwili  hukaa kwenye mapafu na kusababisha mzunguko wa damu kuganda na hatimae kifo.

Kabla ya kifo kirusi hicho  huwa kinasababisha homa kali ya mapafu, ambayo husababisha  mafua makali, mtu kushindwa kupumua  na kuhema .

Waathirika wakubwa wa ugonjwa huo wa mlipuko ni wazee ambao tayari miili yao imepungukiwa na kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali yatakayowashambulia ikiwemo ya mlipuko.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post