BREAKING NEWS : DIWANI MTEULE CCM, WAJUKUU WAFARIKI DUNIA, BAADA YA NYUMBANI KUCHOMWA MOTO.


Diwani Mteule Kata ya Kikongo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoani Pwani, Fatuma Ngozi na wajukuu zake wawili wamekufa baada ya nyumba yake kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo Novemba 9, 2020.


Ngozi ni miongoni mwa madiwani wateule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopata ushindi wa kishindo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,2020.


Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa.


Chanzo : Dira Makini. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post