Tulia kujenga madarasa Mbeya

 

Na Joachim Nyambo,Mbeya

CHANGAMOTO za Uhaba wa vyumba vya madarasa katika Shule ya msingi Nonde na Shule ya Sekondari ya Rejico zilizopo katika kata ya Nonde jijini Mbeya ni miongoni mwa mambo ambayo Mgombea wa Ubunge Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk Tulia Ackson atayapa kipaumbelea kushughulikia iwapo atapewa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao na kuwatumikia wananchi.

Dk Tulia alibainisha hayo katika mkutano wake wa kampeni alioufanya jana katika kata ya Nonde ikiwa ni kata yake ya 32 alizofanya mikutano akiwa amebakiza kata nne huku chama hicho kikiwa na mtaji wa madiwani  16 waliopita bila kupingwa.

Alisema hayuko tayari kuendelea kuona wanafunzi katika shule hizo zenye umuhimu mkubwa jijini hapa wanaendelea kupata shida kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

“Tulikwishaanza kwa kuleta saruji baada ya kutoridhishwa na hali hiyo lakini kule nilifanya kama mbunge wa kujiongeza.Sasa ni wakati wangu kuwatumikia nikiwa mbunge ili tushirikiane kuboresha mazingira ya shule hizi.

“Mimi mbunge wa kujiongeza tayari mmeona tumetoa mikopo ya bajaji,pikipiki na tunaona vijana wamejiajiri kupitia mikopo hii.Sasa kama tuliweza kufanya haya kwa ubunge wa kujiongeza kwa nini tusifanye zaidi nikiwa munge wenu ili nikashirikiane na rais katika mazuri anayolenga kutufanyia hapa Mbeya.”alisisitiza Dk Tulia.

Aidha alisema upo umuhimu mkubwa kwa Mbeya mjini wapigakura kuhakikisha hawatengenezi makande ya uongozi kwa kuchagua watu wa vyama tofauto tofauti bali wachague mafiga matatu na kuwezesha kuwa na uongozi wa kuchaguliwa kuanzia ngazi ya rais,mbunge na madiwani ili kwenye maamuzi wawe na lugha moja.

“Tuchague rais wa CCM,Mbunge wa CCM na Madiwani wa CCM ili tutakapokaa kuzungumzia mradi wa Elimu iwe elimu,tukisema sasa ni afya sote tuelekee huko.Asiwepo kati yetu anayegoma au kutoka nje.”alisema.


 


PIX- Mgombea ubunge jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM Dk Tulia Ackson akinadi sera za chama chake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata ya Nonde.(Picha na Joachim Nyambo)

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post