SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA MAGHALA NA MAABARA YA KISASA KUKABILIANA NA SUMUKUVU

Na Jocktan Agustino,  NJOMBE


Serikali imesema imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi Maghala na Maabara za kisasa za kufanya utafiti wa virutubisho utakaosaidia kukabiliana na tatizo la Sumukuvu nchini utakaoghalimu zaidi ya bil 78 hadi kukamilika kwake.

Mbali na kutenga kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa maghala na maabara , Lakini pia mwezi May 2020 serikali imetenga na kuukabidhi wakala wa chakula nchini NFRA kiasi cha zaidi ya bil 47 kwa ajili ya ununuzi wa nafaka yakiwemo Mahindi,Mtama,Uwele,Mpunga na Ulezi ambayo yanazalishwa kwa wingi mkoani Njombe  na kutoa muongozo wa bei isiwe chini shilingi 500.

Akizungumza wakazi wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya siku ya chakula ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kipindi cha muda mfupi ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo na hifadhi kubwa ya chakula.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akieleza hali ya udumavu amesema Licha ya mkoa huo kuwa kinara wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara lakini Unaongoza kitaifa kwa udumavu nchini kwa asilimia 53.6 na kwamba jitihada za kutoa elimu zimeanza huku lengo likiwa ifikapo 2022 kuwa asilimia 36 ya udumavu.

Lakini Wakazi wa Njombe Wanaitumia vipi Fursa ya kuwa wenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa, Huyo Pindi Chana barozi Mstaafu na Endrew Mwangomile meneja wa yara mikoa ya Njome na Ruvuma wanasema heshima iliyopewa Njombe kuandaa maonyesho kitaifa wataitumia ipasavyo kutoa na kupokea elimu ya matumizi boraya pembejeo na viuatilifu pamoja elimu ya matumizi bora ya lishe ili kuepukana na udumavu

Kauli mbiu -Kesho Njema inajengwa na Lishe Bora Endelevu

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post