DKT.KIRUSWA: NITATENGA MAENEO YA MALISHO KWA MASLAHI YA WAFUGAJI

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Longido mkoani   Arusha Dkt.Stephen Kiruswa akizungumza na wananchi wa kata  ya Mundarara wilayani Longido alipokwenda kuomba kura ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa huko ni wachimbaji wadogowadogo wa madini ya Rubi
Kutoka kushoto ni Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Longido mkoani   Arusha Dkt.Stephen Kiruswa,akiwa na mwenezi wilaya ya Longido
Aliyekuwa  mbunge mstaafu wa jimbo hilo na mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Arusha Mhe.Lekule Laizer akizungumza na wanancji wa kata ya Mundarara wilayani Longido.
Baadhi ya wananchi wa kata ya mundarara waliojitokeza katika mkutano wilayani Longido mkoani Arusha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya mundarara waliojitokez katika mkutano wilayani Longido mkoani Arusha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya mundarara waliojitokez katika mkutano wilayani Longido mkoani Arusha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya mundarara waliojitokez katika mkutano wilayani Longido mkoani Arusha.
Baadhi ya wananchi wa kata ya mundarara waliojitokez katika mkutano wilayani Longido mkoani Arusha.

 

Na.Vero Ignatus,Longido

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Longido mkoani Arusha Dkt.Stephen Kiruswa amesema asilimia 95 ya wakazi wa Longido wanategemea ufugaji  hivyo amesema kwamba watakapomchagua atasimamia na kutenga maeneo ya malisho ili yasivamiwe na wakulima kwa maslahi ya wafugaji

Kiruswa alisema atasimamia na kutetea Sera ya mifugo ambayo hujumuisha shughuli zote zinazohusika na uzalishaji na uendelezaji wa mifugo, Uchungaji, mfumo wa ufugaji ambao mfugaji hutegemea mifugo na mazao yake pekee kukidhi maisha na kujipatia kipato.

Akizungumza katika kampeni iliyofanyika katika kata ya Mundarara wilayani Longido Kiruswa alisema kuwa atasimamia Sera ya uchimbwaji wa mabwawa ,upatikanaji wa maji ya mifugo,madawa,majosho,sambamba na upatikanaji wa masoko

 Aidha Sera hiyo kuhusu huduma ya maji vijijini, inalenga kuboresha afya za wananchi waishio vijijini na kuchangia katika kupunguza umaskini uliokithiri kwa kutoa huduma endelevu ya maji safi, salama na ya kutosha. 

Aidha alisisitiza kuwa atakwenda bungeni  kusimama Sera ya upimaji na urasimishaji wa Nyanda za malisho,kwani Sera hiyo ipo na ilani ya chama chake Cha Ccm  kinaitambua ambapo nyanda hizo ni eneo kubwa ambalo halilimwi na linauwezo mkubwa wa malisho kuhimili mahitaji ya wanyama.
 
Aidha, mfumo huu huendana na desturi ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta maji na malisho ya mifugo. Uendelezaji wa nyanda za malisho Inahusu kuendeleza malisho, maji, matumizi na hifadhi ya nyanda za malisho

Kiruswa alisema atajhakikisha kuwa umeme umeme umefika katika vijiji vyote ndani ya mwaka mmoja na nusu baada ya uchaguzi kwani  mpango wao wa maendeleo unasema utakuwa umefika kila kijiji na kusambazwa kwenye kila kitongoji kwa bei ya shilingi 27,000
Kwa upande wake aliyekuwa  mbunge mstaafu wa jimbo hilo na mwenyekiti mstaafu wa ccm mkoa wa Arusha mhe.Lekule Laizer alimshukuru mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt Magufuli kwa juhudi zake kwa kuruhusu watoto kusoma bure bila malipo, jambo ambalo limeleta usawa kwakaya ambazo zilikuwa za hali ya chini.

Laizer aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha kuwa       wanahifadhi vyema vitambulisho yao vya kupiga kura ili siku ya tararehe 28/10/2020 ikifika wajitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwaajili ya kumchagua kwa wamu nyingine Dkt.Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa CCM kwani wenyewe wameona juhudi na maendeleo aliyoyafanya ndani ya miaka mitano ya uongozi wake.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post