MBEYA CITY YASITISHA MKATABA NA KOCHA AMRI SAID.UONGOZI wa klabu ya Mbeya City umesitisha rasmi mkataba na kocha wake Amri Said baada ya makubaliano ya pande zote mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Mbeya City ambayo kwa sasa inashika mkia katika msimamo wa ligi, itakuwa chini ya kocha msaidizi Mathias Wandiba wakati taratibu za kupata kocha mpya zikiendelea.

"Maamuzi haya yamefikiwa baada ya majadiliano ya pande zote mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu yetu inayoshiriki katika ligi kuu inayoendelea.

"Amry Said alijiunga na timu yetu Disemba mwaka jana tukiwa katika mzunguko wa pili wa michezo ya ligi kuu 2019/2020.

"Klabu inachukua nafasi hii kumshukuru Amry Said kwa kazi yake nzuri na ya kukumbukwa aliyoifanya katika timu yetu katika muda wote aliyohudumu kama kocha mkuu" Ni sehemu ya taarifa iliotolewa na Mbeya City.

Mpaka sasa timu hiyo imecheza mechi 7 , sare mechi 2 na kupoteza mechi 5, haijashinda mechi yoyote.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post