DAWASA KUCHANGIA MATOFALI 2000 UJENZI WA OFISI YA UWAMAKIZI MUHEZA

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi ya Uwamakizi wilayani Muheza wakati wa ziara yao ya siku moja kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange

Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo

Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly katikati akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kushoto wakati wa ziara hiyo kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja wa kwanza kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kushoto akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja kulia wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akieleza namna wanavyotunza mazingira katika vyanzo vya maji kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Dawasa wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis MwamunyangeMwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akieleza jambo kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Dawasa kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) imeahidi kutoa matofali 2000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya umoja wa wakulima wahifadhi wa Mazingira Kihuwi (Uwamakizi) iliyopo Kijiji cha Kimbo Kata Potwe Tarafa ya Amani wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Ahadi hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakati wa ziara yao ya kimafunzo ya siku moja wilayani Muheza ambapo walielezwa jitihada za umoja huo kuanza ujenzi wa ofisi yao kwa nguvu zao.

 Ziara hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) ambapo walitembela maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Bustani ya Uwamakizi katika mlima wa mfano wa shughuli za uwamalikizi.

Alisema wamefika kwenye umoja huo na kusikia jitihada za kuanzisha ujenzi wa ofisi yao kwa nguvu zao wenyewe licha ya jitihada wanazofanya kwenye vyanzo vya maji na wameweza kufyetua matofali 3000.

“Lakini ili nasi tusiondoke hapa bila kuacha kumbukumbu yoyote tumeamua kuchangia juhudi hizo kwa kutoa matofali 2000 kuunga mkono ujenzi wa ofisi hiyo“Alisema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

 Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Uwamakizi Twaha Mbaruku alisema kwamba wana ujenzi wa ofisi na kwa sasa wamekwisha kupata tofali 3200 kwa lengo la kuanza ujenzi.

“Mmekuja hapa tumeshindwa kuwaingiza ofisini tulipokodi kwenye jengo dogo la Serikali kwa sababu ugeni huu hauwezi kuingia lakini tumejiongeza kuona vema tujenge ofisi kubwa”Alisema

Akielezea kuhusu umoja huo Mwenyekiti huyo alisema uwamakizi wataendelea kupambana kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa na kutunzwa ili viweze kuwa endelevu.

 Alisema wao wanachangamoto ndogo lakini wanashukuru Tanga Uwasa tokea walipoanzisha mradi huo 2013 hawakurudi nyuma waliendelea kuongeza mapambano nao na ushirikiano na makubaliano yaliendelea

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post