JOHN BOCCO AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA SIMBA


 Nahodha wa Simba SC, John Bocco amewaomba radhi mashabiki wa Simba SC kwa kupoteza michezo mwili mfululizo ya Ligi Kuu Soka Tanzania bara.

“Wanachama viongozi pamoja na wapenzi wote wa Simba SC kwanza nimshukuru mungu kwa kuwapa moyo wa upendo wana simba wote wakuipenda timu yetu na kuiunga mkono katika vipindi tofauti na kila mkoa tunaokwenda kucheza.”.

Kwa niaba ya wachezaji niseme tunaomba mtusamehe kwa matokeo tuliyopata ya michezo yote miwili iliyopita, tuliteleza na tumeshateleza hatupaswi kuteleza tena na hii ndio ahadi yetu kwenu kurekebisha makosa yetu na kurudi wenye sura mpya na upambanaji mpya kwa michezo yote ijayo ili turudishe furaha yetu kwakupata motokeo mazuri kama tulivozoea tumesha waangusha tunakiri hili ila tunaamini hali hii haitajitokeza tena kwa michezo ijayo,” Nahodha wa Simba SC, John Bocco.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post