BONDIA TYSON NA ANTHONY JOSHUA KUZICHAPA DISEMBA MWAKA HUU.


 Bondia Tyson Fury ambaye ni anashikilia taji la WBC la uzani wa ‘heavy’ atakabana koo na mshindani ambaye atatangazwa hivi karibun jijini London, Uingereza Disemba 5, 2020.

Frank Warren ambaye ni promota wa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema kwamba Fury amefutilia mbali mpango wa kuchapana na Deontay Wilder wa Marekani kwa mara ya tatu mnamo Disemba 2020 na tayari amepata mshindani mpya.


Naye, bondia Anthony Joshua amethibitisha kwamba atashuka dimbani kutetea mataji yake ya kimataifa ya IBF, WBA, WBO na IBO katika uzani wa ‘heavy’ kwenye pigano litakalomkutanisha na Kubrat Pulev wa Bulgaria mnamo Disemba 12 kwenye ukumbi wa The O2 jijini London.


Wawili hao walikuwa wamepangiwa kuchapana makonde katika uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London, Uingereza mnamo Juni 20, 2020 kabla ya shindano hilo kuahirishwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post