WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA HALMASHAURI ILI KUWEZA KUPATIWA 2% YA MAPATO KWA AJILI YA KUWAWEZESHA.

 

SPIKA Job Ndugai ambaye anamaliza muda wake na mbunge wa Jimbo la Kongwa (CCM) ambaye anamaliza muda wake amewataka watu wenye ulemavu kujitokeza katika halmashauri ili kuweza kupatiwa asilimia mbili ya mapato kwa ajili ya kuwawezesha.


Ametoa wito huo leo tarehe 17 Agusti 2020 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Viongozi,Demokrasia na Uchumi dhidi ya Watu wenye Ulemavu uliofanyika kitaifa Jijini Dodoma.


Ndugai amesema kuwa watu wenye ulemavu wanatakiwa kujitokeza kushiriki katika fursa mbalimbali za kimaendeleo badala ya kukaa majumbani au kuishi maisha ya hofu.


Akizungumza na Viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kutoka Tanzania bara pamoja na Visiwani pamoja na wadau mbalimbali amesema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine.


Pamoja na mambo mengine Ndugai amesema kuwa mila na desturi za kitanzania bado zinawakandamiza watu wenye ulemavu kwa kuwaona kama vile hawafai kupata haki zao.


Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya Watu Wenye Ulemavu Tanzania Peter Charles,amesema mkutano huu unalenga kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu ili waweze kujua haki zao.


Amesema mkutano huo unawashirikisha viongozi wote kutoka kwenye vyama vya watu wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo juu kutambua,Uongozi,Demokrasia na Uchumi kwa watu wenye Ulemavu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post