JAMES WARD-PROWSE KUSALIA SOUTHAMPTON MPAKA 2025.

 

Nahodha wa klabu ya Southampton, James Ward-Prowse amesaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kusalia katika klabu hiyo.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na klabu hiyo akiwa na miaka nane na tayari amekwisha tumia misimu nane akiwa ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha Southampton.


Msimu wa 2019-20 akiwa na Southampton alicheza dakika zote kila mchezo na alichukua nafasi ya kuwa nahodha kutoka kwa Pierre-Emile Hojbjerg aliyetimkia Tottenham mwishoni mwa msimu. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post