AOMBA MSAADA WA LAKI8 AFANYIWE UPASUAJI TATIZO LA BUSHA

 Mathayo Kudenya, (25) anaomba msaada kwa wasamalia wema, kumsaidia kiasi cha Sh. 800,000 ili afanyiwe upasuaji wa kutoa maji katika korodani zake, tatizo linalomsumbua kwa zaidi ya miaka mitano sasa.Akizungumza Nyumbani kwao Kudenya, alisema tatizo hilo lilimwanza toka mwaka 2015, na amezunguka katika maeneo mbalimbali bila kupata tiba.

Kudenya, alisema kuwa tatizo hilo lilimwanza mara baada ya kutoka jando mwaka 2015, ambapo alianza kuhisi muwasho na baadaye vikatokea vidonda katika nyonga zake ambavyo vilikuwa vikitoa maji.

“Nilikua nahisi muwasho kwenye korodani zangu muda mfupi vikatoke vidonda katika maeneo ya nyonga vilikuwa vinatoa maji, lakini baada ya kukauka ndipo korodani zikaanza kuvimba na kunyaa maji hadi kufikia hali hii”alisema Kudenya

Pia, Kudenya alisema kutoka na hali hiyo alizunguka katika maeneo mbalimbali hadi kwenda kwa waganga wa kienyeji katika mkoa wa Tanga na kutumia dawa bila mafanikio.

“Nilikwenda kwa waganga Tanga na maeneo ya Chamwino mkoani Dodoma, ambapo wataalamu walinipa dawa bila mafanikio na kunishauri pia niende katika hospitali kubwa ili kubaini nini kinanisumbua”alieleza Kudenya

Kadhalika, alisema kuwa kutokana kuendelea kupata maauvu makali mwaka huu mwezi Aprili, alikwenda katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma, na kufanyiwa vipimo.

“Baada ya kufanyiwa uchunguzi madaktali wamenambia kuwa nina tatatizo la kujaa maji kwenye korodani zangu hali ambayo ninatakiwa kutoa kiasi cha Sh. 800,000 na chupa tatu za damu, ili kufanyiwa upasujai”alisema Kudenya

Aidha, Kudenya alisema kutoka na hali duni ya maisha aliyonayo, hataweza kumudu gharama hizo ambazo ameambiwa kuzilipa ili apatiwe matibabu.

“Mimi hapa nilipo sina wazazi naishi na bibi yangu mwenye umri wa zaidi ya miaka 78, ambaye ndiye namtegemea kunilisha na mimi ambaye ndiye nikuwa msaada wake nimeshindwa kufanya shughuli yoyote kutokana na ugonjwa huu”alisema

Alieleza kuwa, ugonjwa huo umemrudisha nyuma kimaendeleo kutoka na kushindwa kufanya shughuli yoyote ya kujiingizi kipato na kulala kitandani muda wote.

Bibi wa kijana huyo Janeth Mafupi, alisema hivi sasa hali ni mbaya na anawaomba wasamalia wema kumsaidia mjukuu wake ili afanyiwe upasuaji na kurudi katika shughuli zake za kujitafutia kipato kama awali.

Hata hivyo, mjomba wa kijana huyo John Stevene, alisema wao kama familia wameshidwa kumudu ghamala hizo kutoka na hali ya familia hivyo kilio chao ni kwa watanzania wote watakaoguswa kumsaidia kijana huyo.

“Kama kuna mtu ataguswa kutusaidia ili kupata matibabu ya kijana wetu ili arudi katika hali yake ya awali tunaomba awasiline na familia kupitia namba ya simu 0713533337 “alisema  Mjomba huyo


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post