Wanafunzi 16 na Mwalimu Mmoja wajeruhiwa kwa Radi na kuua mmoja


Wanafunzi 16 na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Chief Kidulile iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe wamepigwa radi februari 19 majira ya saa tisa alasiri na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na kuacha majeruhi 16.

Akifafanua kuhusu tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akiwa mkoani Morogoro kikazi amesema amepokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa vijana wake aliowatuma ambapo  amesema katika tukio hilo mwanafunzi mmoja wa kiume kufariki dunia punde baada ya kukimbizwa hospitali na mwingine mmoja kujeruhiwa vibaya mguuni na jichoni huku pia akisema wengine 15 walipata majeraha madogo .

Kutokana na tukio hilo kamanda Issa ametoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhali msimu wa mvua kwa kuto tembea peku,kuweka vizuia radi na kujiepusha na kitendo cha kukaa maeneo matupu ama ya wazi.

Seil Morel ambaye ni mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Ludewa anasema madaktari walipokea watu 17 ambao ni wahanga wa tukio hilo ambapo katika jitihada za kunusuru uhai wao wamelazimika kutoa huduma usiku na mchana hatua ambayo imekuwa na matokeo chanya kwani wanafunzi 15 wameruhusiwa asubuhi akiwemo mwalimu huku pia akidai mmoja amefariki na mwingine mmoja akiendelea kupata matibabu zaidi kwa kuwa amejeruhiwa vibaya .

Dr Morel amesema wanafunzi wakike 11 wamejeruhiwa katika tukio hilo ,wakiume 5 na mwalimu mmoja wa kiume .

Nae mkuu wa shule ya sekondari Chief Kidulile Aloyce Kapelele anasema tukio hilo limeleta mshituko mkubwa shuleni hapo kwakuwa halijawahi kutokea na kwamba jitihada za kuweka vidhibiti radi zinafanyika huku kuhusu wanafunzi walioruhusiwa hospitali wanaendelea na masomo kama kawaida .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post