HATIMAYE JWTZ KUKARABATI BARABARA NDANI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Baada ya taarifa za kusambaa kwa picha zinazoonesha ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo la kitalii la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,mamlaka hiyo imetangaza kuzifunga baadhi ya barabara zinazokwenda katika eneo hilo.

Kwa muktadha huo ili kuzifanyia ukarabati wa kina ili ziweze kupitika na kuondoa sintofahamu ya miundombinu ya barabara  kutokana na uharibifu uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini hivyo kuchukuwa hatua za haraka kudhibiti kadhia hiyo.

 Baada ya kusambaa kwa picha hizo mkuu wa mkoa wa Arusha aliliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata wale waliosambaza picha hizo kwa madai ya kuhujumu uchumi.

 Juhudi hizo za ukarabati wa miundombinu ya barabara za mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya kuongeza suala zima la ubora utakaosaidia wageni wanaotembelea hifadhi hiyo kufika kwenye maeneo yote ya vivutio vya mamlaka hiyo ya hifadhi.

Akiwa katika  Kreta ya Ngorongoro, miongoni mwa vivutio vya kitalii vilivyopo katika hifadhi hiyo, mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Profesa Abiud Kasomila amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ndio watakaohusika kutengeneza miundombinu hiyo.

Alisema kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ndio wataendelea na matengenezo ya barabara kutokana na wao kuwa na uzoefu mkubwa wa masuala hayo na hivyo baadhi ya barabara zitafungwa mpaka pale marekebisho yatakapokamilika.

Hifadhi ya Ngorongoro ina eneo lenye ukubwa wa kilometa 8,300 za mraba lenye mchanganyiko wa aina yake wa sura ya nchi, wanyamapori, wanyama wafugwao na mambo ya kale.

Hifadhi hiyo ni miongoni mwa hifadhi zilizo na vivutio vya kipekee vya kitalii duniani kutokana na kuwa na maeneo maarufu kama vile bonde la Olduvai Gorge ambapo inaaminika fuvu la binadamu wa kwanza lilipatikana hapo.

Ngorongoro Kreta, pamoja na kujumuisha maisha mseto ya wanyama na binadamu,kwa umuhimu huo basi mamlaka ya hifadhi hiyo imeona ni vyema kufunga baadhi ya barabara ili kushughulikia changamoto hizo.

Dkt.Fred Manongi ni kamishina wa mamlaka ya hifadhi hiyoanataja baadhi ya maeneo ya kitalii yatakayofungwa ikiwemo barabara ya kwenda eneo la kreta na maeneo ya Laitol ambayo yamekuwa na changamoto kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Sakata hili lilianzia katika mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha zinazoonesha miundombinu ya barabara kuharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

 Licha ya maagizo ya serikali ya mkoa wa Arusha ya kuwakamata wote waliohusika kusambaza picha hizo,  baadhi ya waongoza watalii wameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kushughulikia suala hilo.

Alisema kuwa changamoto hiyo inaendelea kufanyiwa kazi na watahakikisha wanakamilisha ndani ya muda kuondoa hali hiyo ili wageni waendelee kupata huduma za utalii maeneo yote ya he hifadhi hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post