JESHI LA POLISI ARUSHA LAMUONYA MBUNGE LEMA KUACHA KUINGIA SUALA LA BARABARA ZA NGORONGORO

Na.Ahmed Mahmoud,Arusha

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limesema limepokea maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ya kuhakikisha wachochozi wote pamoja na wanaochafua taswira nzuri ya nchi ya Tanzania wanakamatwa

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoani hapa Jonathan Shanna amesema kuwa wamelipokea agizo hio na kulitekeleza kwa asilimia 100 na watawasaka popote walipo bila kujali nafasi zao walizonazo.

Alisema nimeona Mhe mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akisema anashangaa kuona watu wakikamatwa kwa uchochezi hivyo natumia fursa hii kumtahadharisha akae mbali na suala hili

Alieleza kuwa suala hilo wakati huu ambapo jeshi la polisi linaweledi wa hali ya juu lipo kazini kuhakikisha mkoa unaendelea kuwa salama na utalii unashamiri kila kona  hivyo amemshauri mhe.mbunge asikariri na asome alama za nyakati.

Amemtaka Mhe.Lema kutambua kuwa hii siyo awamu ya mchezomchezo na anaamini kwa pamoja tunaweza uzalendo wetu kwanza na siasa baadae.

Hayo yamekuja baada ya kauli ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyoekeza kufuatiliwa na kukamatwa kwa wale wote wanaosambaza picha za video kwenye mitandao ya kijamii zenye muelekeo wa kuchafua taswira ya miundo mbinu katika hifadhi zetu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post