MAFUNDI SIMU JIUNGENI KWENYE UMOJA TCRA

Mhandisi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kadaya Baluhye akiongea na mafundi wa vifaa vya kieletroniki kwenye mkutano wao na mamlaka hiyo jijini Arusha picha na zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Add capMeza kuu ni Kaimu meneja wa Kanda ya kaskazini wa TCRA Jan Kaaya akiwa na viongozi wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini kwenye mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Sehemu ya mafundi simu kutoka mikoa ya Manyara na Arusha wakifuatilia kwa kina mkutano huo wa mamlaka ya mawasiliano TCRA Kwenye mkutano wa mafundi simu kutoka Kanda ya kaskazini picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Wadau wa sekta ya mawasiliano wakifuatilia mkutano wao na mamlaka ya mawasiliano TCRA wakati walipowataka kuunda umoja wao kwa lengo la kukabiliana na kero mbali mbali picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Wadau wa sekta ya mawasiliano wakifuatilia mkutano wao na mamlaka ya mawasiliano TCRA wakati walipowataka kuunda umoja wao kwa lengo la kukabiliana na kero mbali mbali picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.

Kwa muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundi ambaye atafanyakazi kama hajasoma wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwao kujiunga kwenye kikundi ili kupatiwa elimu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi ndio suluhisho.

Amesema kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini kupitia serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa, Maguwa Manyanda amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii inawategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona umoja ndio suluhisho la changamoto zao.

Amesema kuwa mafunzo hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya Dola.

Alieleza kuwa kufanikiwa ili kila mmoja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.

Nae Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana Mtengeti amesema kuwa wamefurahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo itawasaidia kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na umoja huu.

Awali akitoa mafunzo kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili.

Alisema kuwa jeshi la polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia Ila umoja wenu utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na kuondoa changamoto zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post