MFUNGWA ALIYEKATAA KURUDI URAIANI KWA MSAMAHA WA RAIS ADAI HANA PA KWENDA'Mfungwa Merald Abraham, aliyekataa kurudi Uraiani
Mfungwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Merald Abraham, amekataa kurejea Uraiani baada ya kuachiwa kwa msamaha uliotolewa na Rais Magufuli kwa madai ya kuwa hana pa kwenda na kutaka ahamishiwe katika Gereza la Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Abraham ni miongoni mwa wafungwa 70 katika Gereza la Ruanda, waliopewa msamaha Desemba 9, 2019, na jana  Desemba 10 wakati wenzake wakiachiwa huru, yeye alikataa kubaki huru hali iliyopelekea kujijeruhi usoni, akishinikiza kuendelea kubaki mahabusu.
"Sina pa kwenda, bora nibaki Gerezani, ikiwezekana nitolewe hapa nihamishiwe Gereza la Ukonga Dar es Salaam, ila sio Uraiani" amesema Abraham.
Juzi wakati wa Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania, ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa takribani 5,533 na wafungwa 259 kati yao wanatoka mkoani Mbeya.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post