CHADEMA WAPEWA SAA MBILI KUONDOA BENDERA ZAO BARABARANI DAR


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic ameiandikia barua CHADEMA na kuipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City.

Bendera hizo ziliwekwa takriban wiki mbili zilizopita ulipoanza Uchaguzi wa Mabaraza ya chama hicho huku Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa chama hicho ukitarajiwa kufanyika kesho

Mkurugenzi huyo amesema Manispaa ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za chama hicho zikiwa kwenye bustani

Katika barua ya Mkurugenzi huyo kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji, amesema bendera zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali

Aidha, Meya wa Ubungo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob amesema, “bendera hizo haziondolewi kwa sababu CHADEMA tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi ya Umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post