MBOWE ADAI CHADEMA IMEVUNJA NDOA NYINGI ZA WATU


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema amekuwa akishangazwa na watu wanaohoji kwanini chama hicho kimekuwa kikifanyia mikutano yake katika kumbi zenye bei ghali na kusema kuwa chama hicho hakihubiri umasikini na kwamba wataendelea kuwa juu.


Mbowe ameyabainisha hayo leo Disemba 17, 2019, wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho, unaoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kwamba wao hawataukiri umasikini bali wataendelea kuhubiri utajiri kwakuwa wanachama wake wengi wamepitia maumivu mengi sana.

"Ukumbi wa Mlimani City haututoshi tungetamani tungekuwa na ukumbi mzuri zaidi kuliko huu, lakini hakuna tutabanana humu humu, tuna wivu na chama chetu, tuna wivu kwa sababu kuna watu wana maumivu makubwa, kunawatu wamefungwa, wamepata ulemavu sababu ya chama hichi, kuna Ndoa nyingi zimevunjika shauri ya chama chetu, yote tumeyavumilia sababu tuna ndoto kubwa" amesema Mbowe.

Mkutano huo wa Baraza Kuu la chama hicho, utajadili na kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na kuandaa ajenda za Mkutano Mkuu utakaoanza kesho Disemba 18, 2019.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post