WAZIRI JAFFO APONGEZA MCHAKATO WA UCHAGUZI SINGIDA


 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleimani Jaffo akizungumza na viongozi wa  Mkoa wa Singida jana, kuhusu mchakato mzima wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Angelina Lutambi.
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Waziri Jaffo.
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP)  Sweetbert  Njewike akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano na Waziri Jaffo na viongozi wa mkoa huo ukiendelea .
 
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
 
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleimani Jaffo amewapongeza wakazi wa Mkoa wa Singida kwa kuwa miongoni mwa mikoa mitano nchini iliyoonyesha hamasa na kujitokeza kwa wingi kitakwimu katika suala zima la kujiandikishakwenye daftari la kudumu la mpiga kura, ikiwa ni moja ya hatua muhimu ya mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa unaoendelea.
 
 
Jaffo aliyasema hayo jana mkoani hapa,alipotembelea kukagua utekelezaji wa kanuni na taratibu za mchakato wa uchaguzi huo unavyoendelea hatua kwa hatua.
 
“Katika mchakato huu wa uandikishaji Singida ni miongoni mwa mikoa mitano iliyofanya vizuri sana, na kwa wagombea tayari kwa mfululizo wa siku saba tumekamilisha kuchukua na kurudisha fomu na hatimaye kufanya teuzi kwa wenyeviti na wajumbe wa kamati za rufaa,” alisema
 
Alisema, halihalisi iliyopo mpaka jana ni kwamba jumla ya kata 3956 zilizopo nchi nzima, kimantiki mchakato huo umekwenda vizuri,ingawa kuna baadhi ya maeneo machache zimejitokeza changamoto ikiwemo baadhiya maeneo wagombea hawakupata fomu kwa wakati.
 
Aliyataja baadhiya maeneo hayo kuwa ni Songwe (Vwawa), Arusha (Arumeru), Mwanza na Kilimanjaro (Moshi), huku akizitaka kamati zote za rufaa nchi nzima kuhakikisha wakati wa maamuzi wanasimamia haki na usawa, kwa mujibu kanuni, taratibu na miongozo iliyopo bila ya kumuonea mtu yeyote
 
“Azma yetu sote ni kuona uchaguzi huu unakwenda na unakamilika vizuri kwa lengo mahususi la kuunda mamlaka za serikali za mitaa ambazo zina kwenda kujibu changamoto kubwa za wananchi,” alisema
 
Jaffo alibainisha umuhimu wa mchakato unaoendelea kwa sasa kuwa,uchaguzi huo unakwenda kutengeneza serikali za mitaa zilizo karibu zaidi na wananchi, ambazo taifa likitokana ajenda zozote zile za maendeleo basi utekelezaji na msingi wa maendeleo utatoka chini.
 
Alisema, ifahamike kwa wananchi wote kuwa, kwa mujibu wa kanuni zilizopo,‘Kamatiya Rufaa ya Wilaya’ inaundwa na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ambaye ndiye mwenyekiti, akisaidiwa na wajumbe ambao ni watumishi wanne wa sekta za umma kutoka wilaya zote ndani ya mkoa, huku Katibu  wa kamati naye atatoka ndani ya sekta ya umma lakini yeye tofauti na wenzake, ataruhusiwa kupiga kura.
 
“Mwenyekiti nendeni mkazingatie haki, sikilizeni rufaa na malalamiko yote yatakayo letwa mezani kutoka vyama vyote, na watu wote kwa uhuru na upana wake bila kuingiliwa na mtuyoyote,” alisisitiza Jaffo mbele ya wajumbe wa kamati ya rufaa mkoani hapa, nakuongeza;
 
“mmepewa rungu lisilo kuwa na mashaka…tendeni haki msiogope akikisheni kila kitu kinanyooka, kama kuna mtu anastahili haki mpeni na kama kunakasoro zozote rekebisheni.” 
Zaidi, alilitaka Jeshi la polisi kupitia Makamanda wa mikoa kuendelea kusimamia utaratibu uliowekwa kwa misingi ya amani, na kamwe mtu yeyote asijitokeze kuchafua mchakato wa uchaguzi unaoendelea kwa maslahi yake binafsi.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa mkoani hapa, Wilson Shimo,alisema kwamba wamejipanga vizuri kusikiliza malalamiko na rufaa zote kwa haki na kurekebisha kwa mujibu wa kanuni zinazo waongoza, huku akiweka wazi kuwa mpaka jana bado walikuwa hawaja pokea malalamiko yoyote.
 
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Patrick Zamba,alisema watajitahidi kutoa maamuzi sahihi kwa muda mwafaka kwa mujibu wa sheria na kanuni, kulingana na kutoridhishwa kwao na maamuzi ambayo yamefanyika.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, alisema siku zote ‘siku njema daima huonekana asubuhi’ na kwamba hatua ya mkoa huo kupokea hati ya ushindi na kuwa miongoni mwa mikoa mitano bora ni ishara njema.
 
“Singida ni njema…tena ni njema….na ni njema sana!… asubuhi hii njema ndio itabeba mchana wote kuwa mwema zaidi, kwa hatua zote mpaka kukamilika kwa mchakato mzima wa uchaguzi huu muhimu,” alisema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post