WANAWAKE TABORA WATUMIA UGORO KUPUNGUZA HAMU YA TENDO LA NDOA


Tumbaku inayoelezwa kutumiwa na wanawake mkoani Tabora kuweka katika sehemu zao za siri ili kumaliza hamu ya tendo la ndoa pindi wanapokosa huduma hiyo
Waswahili husema ukistaajabu ya musa utaona ya Firauni, Je unajua matumizi yote ya tumbaku?

Mkoani Tabora nchini Tanzania wanawake wamekua wakitumia Tumbaku ili kupunguza hamu ya tendo la ndoa. Huweka sehemu ya siri kisha kuitoa baada ya muda.

Tabia hiyo imezoeleka sana miongoni mwa wanawake wasio na wenza wao, ikiwemo wajane. Lakini kwa upande wa afya, wako salama?

Wanawake hususani wasio kuwa katika uhusiano na wanaume ama kuolewa hutumia njia kumaliza hamu zao.

''Mimi ni mjane, natumia tumbaku katika kumaliza hamu zangu kwasababu sina mwanaume na wala sitaki mwanaume mwingine, kwa wiki naweka mara mbili'' anasema Zaituni shabani mmoja ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu za siri.

Wanawake wengine nilizunguma nao kama asha, si jina lake halisi anasema kuwa anatumia tumbaku kwasababu alikimbiwa na mwanaume wakati ana ujauzito.

'' kwakeli sitaki kusikia tena wanaume mi nitabaki na tumbaku, mana nikitumia hamu yote inaisha sina haja tena'' anasema asha

Wanawake wote niliozunguma nao wanakiri kuwa matumizi ya tumbaku sehemu za siri huwasaidia kumaliza hamu ya tendo la ndoa.


TUMBAKU INATUMIWA VIPI SEHEMU ZA SIRI?

Kwa mujibu wa wanawake hawa huchukua majani makavu ya tumbaku kisha kutangwa na baada ya hapo huchanganya na mafuta kidogo pamoja na magadi, ama na mara nyingine hutumia ugoro kufanya mchangayiko huo. Baada ya hapo huweka sehemu za siri na kisha hupata muwasho ambao ndio humaliza haja ya tendo la ndoa.

'' mi huwa napaka mara mbili kwa wiki na huwa naweka kwa muda kidogo kabla niondoe na kisha napata muwasho, na wala sipati maumivu yoyote nikimaliza matamanio yangu ya kufanya tendo la ndoa yanakua yameisha'' anasema zaituni.

Kwa kawaida wanawake hawa baada ya kupaka tumbaku ama ugoro sehemu za siri husikia kama wamekutana kimwili na wanaume.
 Wanawake hawana uelewa wa kutosha kuhusu athari za tumbaku


WANAUME WANASEMA NINI?

Katika kijiji cha ugala suala hili ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake lakini kwa upande wa wanaume si wengi wanajua , na wanaojua wanasema kuwa imekua siri baina ya wanawake.

"Mimi nimekua nikisia lakini mara nyingi ni kwa bahati mbaya wao wakiongea, na nikuwaliza , wanasema ni siri yao ni baina ya wanawake na si wanaume". Anasema mzee Usantu mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ugala.


KUNA ATHARI ZOZOTE KIAFYA?

Kwa mujibu wa baadhi ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu zao za siri, wanasema hawajawahi kupata tatizo lolote kiafya.

Lakini mtaalamu wa magonjwa ya akina mama anasema kuwa baadhi ya wanawake wanaokutwa na viashiria vya saratani hasa ya kizazi wamekua na historia ya kutumia tumbaku sehemu za siri

"Hatuna utafiti wa moja kwa moja lakini data za kwetu hapa wakati tunawahoji tabia za mazoea walizonazo baadhi wamekiri kutumia tumbaku , hivyo hiyo inaweza kuwa miongoni mwa sababu na kama viashiria vingine vikiwepo" anasema daktari.

Matumizi haya ya tumbaku kwa asilimia kubwa yamechangiwa na uelewa mdogo wa wanawake wa kijiji cha ugala, juu ya madhara ya kiafya wanayoweza kupata.

BBC

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post