ACT WAZALENDO WAFUATA NYAYO ZA CHADEMA, WAJIONDOA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam 
 
Chama kingine cha upinzani chenye ushawishi nchini cha ACT Wazalendo kimejitoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 24 Novemba 2019.
zitto
Zitto Zuberi Kabwe, kiongozi mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania


''Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. 

Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.'' Anasema Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT wazalendo katika mkutano na waandishi wa habari.
  
Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa ilikutana jana Novemba8, 2019 kujadili hali na mwenendo wa uchaguzi huo nchini Tanzania. 

Lakini pia chama hiko kimedai kutumika vibaya kwa jeshi la polisi la nchini Tanzania kuingia mchakato wa uchaguzi huo.

bendera
bendera ya chama cha ACT ikipepea

''Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.'' Anaongeza Zitto Kabwe katika taarifa yake.

Mapema jana, Mbunge huyo Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo aliandika  katika ukurasa wake wa twitter kuomba ushauri kwa umma kuwa wachukue hatua gani? katika mchakato unaondelea wa serikali za mtaa?

Zitto Kabwe alitoa kauli hiyo mara baada ya chama kikuu cha upinzani nchini Chadema kutangaza kuwa kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha serikali  Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi imesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu.

Ufafanuzi huo umetolewa mapema jana  katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni, Dodoma ambapo Mbunge wa Singida Kaskazini Justice Monko alitaka ufafanuzi wa serikali hasa baada ya Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato wa Uchaguzi huo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post