WAFANYAKAZI HOTELI YA NAURA SPRING WAMLILIA RAIS MAGUFULI, WATUHUMU IDARA YA KAZI ARUSHA

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, ARUSHA

Wafanyakazi zaidi ya 100 wakiwemo 22 waliofukuzwa kazi hivi karibuni bila kulipwa stahiki zao, na uongozi wa hoteli ya Naura Spring Jijini hapa wamemwomba Rais John Magufuli kusikia kilio chao cha muda mrefu baada ya kukosa msaada kwa uongozi wa mkoa kutokana na mkurugenzi wa  hotel hiyo, Randy Mrema kudaiwa kuwaweka mfukoni

Wakiongea kwa masikitiko baadhi ya wafanyakazi hao waliodai kufanyakazi kwa zaidi ya miaka kumi,wamesema kuwa uongozi wa hotel hizo uliwaandikia barua ya ukomo wa ajira Ifikapo oktoba 31 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni kampuni kushindwa kujiendesha .

"Kutokana na hatua hiyo walipaswa kuandaa malipo yetu ikiwemo mishahara ya miezi minne tunayoidai ,makato ya NSSF na malipo ya kusitisha ajira kuliko walivyofanya kwa sasa na kusababisha familia zetu kuteseka kwa njaa,"walisema.

Wakiongea kwa niaba ya wenzao baadhi ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi, Grayson Mwanga na Kisuno Bernard wamedai kwamba uongozi wa hotel hizo umeshindwa kuwalipa stahiki zao na wamekuwa wakiwadharau wafanyakazi pindi wanapoulizia malipo ya mishahara yao.

"Hapa tulipo hatujalipwa mishahara ya miezi minne ,makato ya mfuko wa hifadhi nssf ambayo wamekuwa wakikatwa kila mwezi lakini mwajiri wao hapeleki kwenye mfuko huo jambo ambalo tunataka rais Magufuli aingilie kati" Wamesema Mwanga.

Wamemtuhumu mkurugenzi wa Hotel hizo,Randy Mrema kuwa na mahusiano na viongozi wote wa mkoa wa Arusha ,wakiwemo wa idara ya kazi jambo ambalo wamekosa mtu wa kusikiliza kilio chao na hivyo kumtaka rais Magufuli,TAKUKURU idara ya usalama,waziri mwenye dhamana, kuingilia kati kuchunguza jambo hilo.

"Awali Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro alitusaidia sana na kuwezesha kulipwa kwa mishahara ya nyuma lakini naye kwa sasa amejiweka kando na suala letu hali ambayo tumekosa mtu sahihi wa kutusaidia" Alisema Mwanga

Akiongea sakata hilo afisa wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdumi anayedaiwa kuwekwa mfukoni na mkurugenzi wa hotel za Impala na Naura, amekanusha kurubuniwa kwa kitita cha fedha na kigogo huyo ili apindishe haki ya walalamikaji,ila amesema kuwa suala hilo analishughulikia kwa umakini mkubwa kwa mujibu wa Sheria za kazi.

" Tumefanya mazungumzo na uongozi wa hotel hiyo na kutoa maelekezo lakini kumekuwepo na suala la utovu wa nidhamu kwa wamiliki wa hotel hizo kukiuka makubaliano ya wazi"Amesema Mdumi

"Ofisi yangu imewashauri wafanyakazi hao pamoja na wale walioachishwa kazi kufungua kesi mahakamani kulalamikia kuachishwa kazi bila kupewa stahiki zao ikiwemo kukatwa makato ya mfuko wa hifadhi wa NSSF bila kupelekwa katika mfuko huo"amesema Mdumi

Wanahabari walipomtafuta Mkurugenzi wa hotel hizo RANDY MREMA kupata ufafanuzi wa jambo hilo ,mkurugenzi huyo hakutoa ushirikiano badala yake alitimua mbio na kuingia kwenye gari lake la kifahari na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha waandishi waliokuwa wamejazana katika hotel ya Impala wakishangaa

Amesema mpaka sasa wamepeleka maombi Mahakamni kuomba itoe amri kukamatwa kwa Mali za kampuni hizo ili iweze kulipa mishahara baada ya kushindwa kutekeleza Maelekezo ya Idaya ya kazi mpaka sasa kampuni hizo zina kabiliwa na kesi namba 83 / 2019/ kwa Naura Spring na Impala kesi namba 84 / 2019 kwa impala Hotel 
  Afisa wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdumi  akiwa ofisini kwake 

 baadhi ya wafanyakazi wakionyesha barua walizosimamishiwa nazo kazi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post