RAIS MAGUFULI KUTUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA KESHO

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kesho kitamtunukia Rais Dk. John Magufuli Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa (Honorary PhD) kwa uongozi wake hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kuwekeza kwenye elimu, miundombinu, kuimarisha utawala bora, na mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 20, 2019 makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema shahada hiyo itatolewa kesho katika mahafali ya 10 ya chuo hicho.
 
Profesa Bee amesema wahitimu 6,488 watatunukiwa astashahada, shahada, stashahada ya juu, shahada ya umahiri, na shahada ya uzamivu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post