RAIS DKT MAGUFULI AWEKA REHANI AJIRA ZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WALIOKOPA BENKI, AWATAKA WALIOKWISHA KOPA WAZIREJESHE KABLA HAWAJAFUKUZWA KAZI


AJIRA za wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji nchini ni sawa na kusema ziko hatarini baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuacha  mara moja kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa madai ya kufanya miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli amesema endapo kama kuna Mkurugenzi amekopa fedha  kwaajili ya kufanyia miradi ya maendeleo na bado hazijaanza kutumika azirudishe mapema na kama hatofanya hivyo atakuwa amejifukuzisha kazi.

Ametoa kauli hiyo Jumatano Novemba 27, 2019 wilayani Bukombe mkoani Geita wakati akihutubia mkutano wa hadhara, Rais Magufuli ambapo amewaagiza hao ambao wameshakopa kuzirudisha na kuvunja mikataba waliyoingia.

“Kama kuna mkurugenzi yeyote amekopa fedha azirudishe, mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya Serikali ni paymaster general wa Serikali ambaye ni Wizara ya Fedha pekee.”

“Anayekopa ajiandae kutoka. Naamini Wakurugenzi wamenielewa, nimepita Kahama Mkurugenzi ananiambia anataka kukopa kutoka TIB (Benki ya Uwekezaji Tanzania) kwa ajili ya kujenga stendi, haiwezekani fedha za wananchi kuchezewa, ovyo”  alisema Rais Magufuli

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post