MKUU
wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wenyeviti wapya wa
vijiji na vitongoji wilayani humo kuacha kujshughulisha
na biashara za magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua
wahusika ili
kukomesha vitendo hivyo.
Mark aliyasema hayo wakati akifungua mkutano
wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa
kodi kwa hiari.
Alisema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi
ya Kenya hivyo ikiwemo ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa
vitendo vya namna hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na
kutokuviruhusu kwenye maeneo yao.
“Ndugu zangu wevyeviti wa vijiji na vitongoji acheni
kushirikia kwenye vitendo vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo
tunaikosesha serikali mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za
kimaendeleo lakini pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea
kushirikiana na TRA kufanya operesheni za kupambana na vitendo vya biashara
haramu za magendo ili kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo
la Horohoro wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha
bandari ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.
Alisema kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali
kupata kodi huku akieleza wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo
watakuwa wamekwisha kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia
halali za kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.
,dc akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia
wafanyabiashara kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na
kwamba kila kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara
kutangaza biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja
na hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi
Awali akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga
Salim Bakar alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa
kodi kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na
kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi mbalimbali
inatekelezwa kupitia kodi hizo.
Naye kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally
Ally amesema umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba
maendeleo yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.
“Mimi kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea
kuhakikisha ninahamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia
kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo “Alisema
Hata hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya
wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara
kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.