NAIBU WAZIRI KANYASU ASISITIZA MAHUSIANO MEMA KATI YA WANANCHI NA HIFADHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda miaka 30 kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha ambapo Mhe. Kanyasu amewataka wahifadhi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, Aidha,amewataka wananchi waheshimu sheria za uhifadhi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika kitongoji Momella mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt. John Pallangyo wakizungumza na Wakuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha mara baada ya kuwasili katika ofisi za Hifadhi hiyo kabla ya kwenda kuzungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda miaka 30 kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kitongoji hicho mkoani Arusha.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt. John Pallangyo akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda miaka 30 kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kitongoji hicho mkoani Arusha.
…………………..

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka  Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Arusha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria bila kuwanyanyasa wananchi.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewataka  wananchi kuzingatia sheria za uhifadhi ikiwa pamoja na kushiriki katika kulinda Hifadhi hiyo
 

Ametoa kauli hiyo leo  wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha  Momela kata ya Ngarenanyuki katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
 
Hatua hiyo inakuja kufuatia mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 30 baina ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Wananchi wa Kitongoji cha Momella wanadai kuwa  mwaka 1992,Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilimega  hekta 600 ya  ardhi ambayo ilikuwa inamilikiwa na Kitongoji hicho, Licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani hawajarudishiwa Ardhi yao hadi leo.
 
Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa Serikali inautambua mgogoro huo na ni miongoni  mwa  migogoro 1000 inayofanyiwa kazi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi.
 
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi hao kuendelea kuwa watulivu hadi pale Serikali itakapotoa orodha ya majina ya vijiji na vitongoji ambavyo vitakuwa vimeondolewa kwenye Hifadhi nchini.
 
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaatahadharisha wakazi wa Kitongoji hicho kutokuingiza mifugo ndani ya  Hifadhini kwa kisingizio cha mgogoro huo.
 
Kwa Upande wake Mbunge wa Arumeru, Dkt.John Pallangyo amewasihi wananchi kuendelea kuzingatia sheria za Uhifadhi huku wakisubili orodha ya majina ya vijiji na vitongoji vitakavyotangazwa kuondolewa katika Hifadhi nchini.
 
” Natambua mna uchungu na mmeteseka kwa muda mrefu juu ya  Mgogoro huu, Niwahakikishie Waziri kawasikia na kajionea mwenyewe” alisisitiza Mhe.Pallangyo
 
Awali akizungumza kwenye  mkutano wa hadhara, Mwenyekiti  wa Kitongoji hicho, Anael Nko amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa kwa muda miaka 30 sasa maisha yao yameendelea kuwa ya uhasama kati yao na  Hifadhi
 
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti huyo amemuomba Naibu Waziri  kuumaliza  mgogoro huo kwani umekuwa ukiwarudisha nyuma kimaendeleo 
 
Mbali na hilo, Mwenyekiti alisema licha ya mgogoro huo wanaihitaji Hifadhi kwa vile licha ya changamoto hizo wanazokumbana nazo Hifadhi hiyo imekuwa na manufaa makubwa sana  kwao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post