MCHUNGAJI RWAKATARE 'MAMA KISULISULI' ASEMA VIJANA HAWATAKI KUOA KUKWEPA MAJUKUMU,WENGI NI MARIOO

Mama wa upepo wa kisulisuli na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Dkt Getrude Rwakatare, ameeleza sababu ya wanawake wengi kushindwa kuolewa ni kutokana na vijana wengi kukwepa majukumu yao.
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital,Askofu Dkt Getrude Rwakatare, amesema kila mtu lazima aolewe na kuoa sio vijana kukwepa majukumu na kukimbilia kuwa Marioo.
"Tatizo la wanawake kukawia kuolewa ni tatizo la kidunia, ulimwenguni kote kuna tatizo kama hilo kwa sababu Wanawake tupo wengi kuliko wanaume, lakini tatizo hili limekuwa kubwa zaidi kwa sababu vijana wanakwepa majukumu yao ndiyo maana inakuwa shida" amesema Mama Rwakatare.
"Vijana wa sasa hivi wengi wanakwepa majukumu hawataki kujiingiza kwenye shida wengi wao ni "Marioo" wanataka kuolewa na majimama hii mbaya sana na ndoa ni mipango ya Mungu" ameongeza.
Aidha Mama Rwakatare, amesema ndoa hazidumu kwa kuwa watu wanakaa mwaka mmoja, mitatu au wengine ni miezi sita kisha zinakufa kwa sababu maadili hakuna na sasa hivi watu wanaoana kwa 'fashion'.

 Chanzo - EATV

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post