MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA, SWEDI MKWABI AJIUZULU


Uongozi wa klabu ya Simba unatoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote kwamba Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kwa uamuzi wake mwenyewe amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Swedi ameiandikia Barua Bodi ya Wakurugenzi kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mohammed Dewji, ambapo ameeleza sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba pamoja na Sekretarieti ya Simba imemtakia kila la heri katika shughuli zake.

Lakini pia imeeleza kuwa ina imani ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Aidha imebainisha kuwa utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya utatangazwa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post