Dkt. Mwakyembe Atembelea Shule Yenye Vipaji vya Michezo ya Orkeeswa Monduli

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Orkeeswa iliyopo Wilaya ya Monduli Jijini Arusha alipowatembelea jana , ambapo alipata fursa ya kuona vipaji vya michezo mbalimbali inayofanywa na wanafunzi hao.Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mwenye kofia) akipata maelekezo kuhusu wachezaji wa mpira wa kikapu (hawapo katika picha) kutoka kwa Mkurungezi wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa Bwana Peter Luis (kulia) alipoitembelea jana Wilaya ya Monduli Jijini Arusha pembeni ya Waziri ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bwana Robert Siyantemi.Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia vikombe mbalimbali walivyoshinda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa katika mashindano waliyowahi kushiriki ndani na nje ya nchi.Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni wachezaji wa mpira wa kikapu (BasketBall) wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa jana Wilayani Monduli Jijini Arusha.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post