Man United yaiadhibu Chelsea huku Arsenal ikipata ushindi mwembamba dhidi ya Newcastle

Rashford baada ya kufunga mkaju wake wa penalti
Marcus Rashford alifunga magoli mawili huku Man United ikianza msimu wake vizuri kwa  kujipatia ushindi wake wa kwanza mnono katika mechi yake ya ufunguzi msimu huu dhidi ya Chelsea katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford. 

Mshambuliaji huyo wa England aliiweka kifua mble United kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa na beki Kurt Zouma.
Beki mpya wa United Harry Maguire alipata mpira ambao ulisababisha bao la pili lililofungwa na Anthony Martial.
  • 'Neymar akaribia kuihama PSG'- Je anaelekea wapi?
  • Tetesi za soka Ulaya Jumapili 11.08.2019:
  • Msimu mpya, kuna jipya?
Wakati huohuo Rashford aliifunguia goli la tatu timu yake kabla ya mchezaji mpya Daniel James kufunga goli la nne na kumwacha mkufunzi mpya wa Chelsea Frank Lampard bila jibu.
Chelsea walitawala mpira na kukosa mabao ya wazi kupitia Tammy Abraham aliyegongesha mwamba wa goli kabla ya Emerson palmieri kupiga juu ya mwamba baada ya penalti ya Rashford.
Hata hivyo United ilichukua udhibiti wa mchezo baada ya kipindi cha kwanza na kupata ushindi wake mkubwa nyumbani dhidi ya Chelsea tangu 1965.

Wakati huohuo Pierre-Emerick Aubameyang aliadhibu masikhara ya Newcastle iliokuwa ikilinda lango lake na kuipatia Arsenal ushindi katika uwanja wa St James' Park. 

Pierre Emrick Aubameyang alifunga bao la pekee
Licha ya kuanza na wachezaji wake wengi waliosajiliwa katika dirisha la uhamisho wakiwa kama wachezaji wa ziada na wakiwa bila Mesut Ozil na Sead Kolasinac , mkufunzi wa Gunners Unai Emery alitazama kikosi chake kikishindwa kupenya katika upande wa upinzani katika kipindi cha kwanza.
Hata hivyo hayo yote yalibadilila kabla ya kipindi cha mapumziko wakati Aubameyang alipowachwa pekee karibu na eneo hatari , akachukua pasi ya Ainsley Maitland-Niles upande wa kulia na kumfunga kipa Martin Dubravka.
Emery alimuingiza mchezaji ghali wa klabu hiyo Nicolas Pepe na kiungo wa kati Dani Ceballos lakini hawakuweza kung'ara.
Upande wa Newcastle Mshambuliaji wake aliyevunja rekodi ya timu hiyo Joelinton alikaribia kufunga lakini kipa Bernd leno akaudaka mpira huo huku shambulio la Jojo Shelvey likigonga mwamba wa goli.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post