Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 12.08.2019 : Chilwell, Pogba, Coutinho, Neymar, Ozil, Lovren

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Leicester City Ben ChilwellKocha Kocha wa Chelsea Frank Lampard anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi kutoka Leicester Ben Chilwell, marufuku ya kufanya uhamisho itakapokwisha, mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England, 22 ana thamani ya pauni milioni 70(Sun)

Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaansa, Paul Pogba, 26, anasema kuna swali wakati wote kuhusu mustakabali wake ndani ya Manchester United (RMC - in French)

Barcelona wanasema winga timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho hataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Marca)

 Neymar

Mazungumzo kati ya Barcelona na Paris St-Germain kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Neymar yamesimama huku klabu hiyo ya Ufaransa ikiomba wachezaji watatu zaidi kufidia gharama ya mchezaji huyo. (Sport)

Wawakilishi wa kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, 30, watasafiri kwenda Marekani kufanya mazungumzo na DC United kuhusu uhamisho wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani. (Express)

Roma bado inataka kumsajili beki wa kati wa Liverpool na timu ya taifa ya Croatia Dejan Lovren, 30. (Corriere dello Sport)
 Paul Pogba


Barcelona itamruhusu Rafinha ambaye alikuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Liverpool na Arsenal- kuondoka kwenye klabu hiyo wakati Valencia ikiwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo wa Brazil, 26. (Sport)

Kocha wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Jose Mourinho amesema kikosi cha pili cha Manchester City kitashinda, kikiongoza moja kati ya timu zake za zamani au Arsenal. (Telegraph)

Kiungo wa zamani wa Tottenham na West Brom Nacer Chadli, 30, ameungana na Vincent Kompany kwenda Anderlecht kwa mkopo akitokea Monaco.(Anderlecht official website)

Mshambuliaji wa Bristol City Matty Taylor, 29, yuko kwenye hatua za mwisho kuhamia Oxford United. (Bristol Post)

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 11.08.2019:
Juventus haijapoteza hamu ya kumsaini kiungo wakati wa Man United Paul Pogba, 26. (Express)
Pogba anasisitiza kuwa hataleta mgawanyiko miongoni mwa wachezaji licha ya madai kwamba alitaka kuondoka Trafford. (Mirror)


Filippe CoutinhoParis St-Germain ina hamu ya kuafikia mkataba utakayoifanya Real Madrid kumnunua mshambuliaji wake raia wa Brazil Neymar, 27, kutoka kwao kwa dau la £149m mbali na klabu hiyo kuikabidhi kiungo wake wa kati raia wa Croatia Luka Modric, 33. (Times - subscription required)

Beki wa Tottenham Serge Aurier anataka kuondoka katika klabu hiyo huku AC Milan na klabu yake ya zamani PSG zikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Coast . (Mail)

Manchester United hawana hakika iwapo mlinda lango David de Gea atatia saini kandarasi mpya . Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 inakamilika msimu ujao na raia huyo wa Uhispania yuko huru kuanza mazungumzo na klabu za kigeni mwezi Januari(Mirror)

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post