KULEA YATIMA SIO JUKUMU LA WAFADHILI: KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII
Na Woinde Shizza, APCBLOG, ARUSHA

WATANZANIA wametakiwa kubadilika na kuanza kuwatunza watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi na kuondoa dhana ya kuwa jukumu la kuwaleta watoto hao ni la wafadhili kutoka nje ya nchi.

Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha leo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi amesema kuwa dhana ya kuliacha kundi hili kutunzwa tu na wageni kutoka nje ya nchi haileti taswira nzuri.

Dkt.Ng'ondi amesema ni vyema watanzania wakajenga utaratibu wa kuchangia Kundi hili ili kupunguza baadhi ya changamoto badala ya kuwaachia wageni kutoka nje.

"Hii dhana haileti taswira nzuri Jamani tumekuwa tukiwaachia wageni tu kuchangia kuanzia masomo , chakula,na mengineyo kwanini hatujishughulishi na hawa watoto wakati ni watanzania "alihoji dkt.Ng'ondi

Hata hivyo aliitaka kamati ya ulinzi kwa watoto Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu Juu ya ukatili kwa mtoto kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa vitendo hivyo vimekidhiri katika mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani na Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani Mendert Schaap amesema kuwa kituo hicho kinalea watoto zaidi ya 300 na kuwapatia elimu na kuwakutanisha na wazazi wao.

Bw.Schaap amesema kuwa mbali na kuwawezesha watoto wanaoishi mitaani makazi hayo Salama,yatawawezesha watoto kupatia misaada mbalimbali na kujiendekeza kiuchumi na kielimu.

Mmoja wa watoto aliyeokolewa mtaani anayefahamika kwa jina la Marry Christopher (19) amesema kuwa aliingia mtaani akiwa na miaka kumi tu na aliweza kuishi ndani ya miaka miwili mtaani Kama mtoto wa kiume ili aweze kukwepa vitendo vya ukatili.

Marry amesema kuwa kituo cha Amani kimeweza kumpatia elimu na Sasa ni mwalimu ambaye anafundisha kuchomelea vitu Mbali Mbali na kuwataka watoto wa mitaani pindi wanapokolewa kutumia vyema nafasi ya elimu na kupata ujuzi .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post